Tuesday, April 24, 2018

WAZEE WA KIMILA TARIME WAUNGANA KUONDOA MIIKO INAYOMKANDAMIZA MTOTO WA KIKE


Wazee wa Mila koo 12 Wilayani Tarime Mkoani Mara Wameungana kwa pamoja kwa lengo la kuzungukia Koo hizo ili kutoa tamko la kuondoa Miiko ambayo imekuwa ikikandamiza Mtoto wakike ambaye hajakeketwa, Baadhi ya Miiko hiyo ni kama kufungua zizi,(Kihita) Kutoruhusiwa kuchangamana na wenzake katika Sherehe za Kijamii na kuitwa Likunene kwa sababu hajakeketwa.

Wazee hao sasa wameanza zoezi la kuzungukia koo hizo 12  huku wakikutana na jamii kwa lengo la kutoa tamko sasa la kuondokana na Miiko hiyo ili mtoto wa kike ambaye hajakeketwa aweze kuthaminiwa kama watoto wengine katika jamii inayomzunguka.

Muungano wa Koo hizo ni Bwirege, Nyamongo, Nyabasi Butimbaru,Bukira, Renchoka, Bunchari,Buhunyaga,Bumera,Watobori, Wasweta na wakenye sasa wameungana kwa pamoja kwa lengo la kutoa Tamko ili kuondoa Miiko hiyo.

 Mwita Nyasibora ni Katibu Msaidizi wa Muungano wa koo 12 za kabila la kikurya Tarime amesema kuwa watazungukia koo zote hizo na kukutana wa wananchi katika Mkutano wa hadhara na kutoa Tamko la pamoa.

“Mashirika yametoa elimu sana likiwemo shirika la ATFGM Masanga na sisi wazee tumeamua kuungana ili kuondoa suala zima la Ukeketaji kwa mtoto wa kike bali tutapaka Unga na kuondoa Miiko hiyo” alisema Mwita.

Maria Nyamboge ni mmoja kati ya waliokuwa ngariba baada ya kupata Elimu juu ya madhara ya Ukeketaji sasa ameachana na suala hilo na anadai kuwa kile kilikuwa kipato chake sasa ameiomba Serikali kumpa mtaji ili kufanya biashara za kuingiza kipato huku Kaimu Afisa Mtendaji kata ya Matongo Joyce Mbusi akiomba wazee wa Mila hao kuabadilika na kuewndelea kuondoa Miiko inayokandamiza Mtoto wa kike ili apate haki zake za Msingi na siyo Kukeketwa.

Kwa Upande wake Valerian Mgani ambaye ni Meneja Miradi Shirika la ATFGM Masanga lililopo Tarime ambao wanapiga suala la Ukatili wa kijinsia ukiwemo Ukeketaji amesema kuwa baada ya kutoa Elimu ya kutosha kwa wazee hao sasa wameamua kuamka na kupaza  Sauti ya Pamoja ili jamii iweze kuondokana na Miiko ambayo inazidi kumnyima haki Mtoto wa Kike.

“Sisi kama Shirika tunaona tayari mabadiliko yameanza kupatikana kama wazee wameungana na sasa tunazunguka nao kwa ajili ya kutoa tamko lao la kuondoa Miiko ambayo imekuwa chanzo cha msichana kwend kukeketwa ili kuendana na jamii” alisema Valerian Mgani.

No comments:

Post a Comment