TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imebainisha jumla ya vyuo 52 vyenye
wanafunzi zaidi ya 7,936, ambao wamedahiliwa katika programu ambazo
hawana sifa.
Taarifa iliyotolewa kwa umma na Katibu Mtendaji wa TCU, imesema tume
hiyo imekamilisha uhakiki wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo
kwenye baadhi ya vyuo vya elimu ya juu nchini.
Aidha, taarifa hiyo imebainisha kuwa orodha ya wanafunzi wasio na sifa imeshawasilishwa kwenye vyuo husika.
“Hivyo wanafunzi wote wanaoendelea na masomo kwenye vyuo vya elimu ya
juu nchini wanaweza kutazama matokeo ya uhakiki wao kupitia tovuti ya
tume,” ilisema taarifa hiyo kupitia tovuti ya tume hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya TCU, wanafunzi wote waliobainika kukosa
sifa hizo, wawasiliane na vyuo vyao ili kuthibitisha sifa zao kabla ya
Februari 28, mwaka huu.
“Kwa wanafunzi ambao hawatahakiki taarifa zao v
yuoni mwao, hawatatambuliwa na TCU na hivyo kukosa sifa za uanafunzi,” ilifafanua taarifa hiyo. Katika tovuti hiyo, jumla ya vyuo vikuu 52 vilihakikiwa ambapo zaidi ya wanafunzi 7,936 walibainika kudahiliwa katika programu ambazo hawana sifa nazo.
yuoni mwao, hawatatambuliwa na TCU na hivyo kukosa sifa za uanafunzi,” ilifafanua taarifa hiyo. Katika tovuti hiyo, jumla ya vyuo vikuu 52 vilihakikiwa ambapo zaidi ya wanafunzi 7,936 walibainika kudahiliwa katika programu ambazo hawana sifa nazo.
Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (AJUCO) wanafunzi 27,
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) 96, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) 224, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) 52,
Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira Kampasi ya Dar es Salaam 74, Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo (SUA)164.
Vyuo vingine ni Chuo Kikuu cha Askofu Mkuu Mihayo Tabora (AMUCTA) 33,
Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) 23, Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro
(MUM) 162, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Must)11, Chuo
Kikuu cha Mzumbe 639 na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) 44.
Vingine ni Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) 115, Chuo Kikuu cha Mtakatifu
Augustine (SAUT) 1,046, Chuo cha SAUT Arusha mmoja, Chuo Kikuu cha
Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) 150, chuo cha Udaktari cha St
Francis Ifakara(SFUCHAS)76 na College of Management and Commerce
(SJUCMC) mmoja.
Aidha, vyuo vingine ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano
Moshi (SMMUCo) 15, Chuo Kikuu cha St John’s Tanzani (SJUT) 968, Chuo cha
St Marks 129 na Chuo cha Udhibiti na Usimamizi wa Wanyamapori (CAWM)
wanafunzi sita.
Katika tovuti hiyo pia vyuo vingine vilivyohakikiwa na kubainika kuwepo
kwa wanafunzi hao ni Chuo Kikuu cha SUMAIT 552 na Chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE) Dodoma 375 na CBE Mwanza 101, Chuo cha Maendeleo ya Jamii
(CDTI) 14 na Chuo cha Diplomasia (CFR) 14.
Vyuo vingine ni Chuo cha Bugando (CUHAS) wanafunzi 36, Chuo cha
Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo cha Bahari (DMI) wanafunzi wanne,
Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EAST C) 20, Chuo Kikuu cha Tanga
Eckernforde (ETU) watatu na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Herbert
Kairuki 12.
Aidha, wanafunzi wengine waliohakikiwa na kubainika kudahiliwa katika
programu ambazo hawana sifa nazo walipatikana katika vyuo vya Chuo cha
Uhasibu Arusha (IAA) wanafunzi 56, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
305, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU) 149 na Chuo
cha Ustawi wa Jamii (ISW) 116.
Vyuo vingine ni Chuo cha Kodi (ITA) wanafunzi sita, Chuo Kikuu Kishiriki
cha Jordan (JUCO) 186, Kilimanjaro Christian University College
(KCMUco) 55, Chuo Kikuu cha Kenyatta, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
(Muco) 62, Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar (ZIFA)(20) na Chuo Kikuu
cha Bagamoyo wanafunzi 53.
Vingine ni Chuo cha Tumaini Makumira (TUMA) wanafunzi 208 waliokutwa
hawana sifa katika programu wanazosomea, TUMA-Mbeya 11, Chuo Kikuu cha
Iringa (UOI) 522, Chuo Kikuu Sumait 552, Chuo Kikuu cha Teofil Kisanji
(TECU) Dar es Salaam watatu, Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Maris
(STEMMUCO) 44 na Chuo cha Mipango wanafunzi 431.
No comments:
Post a Comment