.

.
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Wednesday, October 4, 2017

TAZAMA PICHA:TOP 5 YA MASTAA WA MUZIKI AFRIKA WENYE FOLLOWERS WENGI INSTAGRAM

Davido

 Msanii kutokea nchini Nigeria David Adedeji Adeleke maarufu kama Davido aliyetamba na ngoma yake ya “Fall” iliyofanya vizuri Afrika na Duniani kwa ujumla, Davido ndio msanii mwenye mashabiki wengi kwenye mtandao wa instagram (Milioni 5) katika Bara la Afrika.

Nafasi ya pili inafuatiwa na msanii kutokea Nigeria pia Wizkid Ayo maarufu kama star boy mwenye mashabiki million 4.1 kwenye kurasa yake ya instagram, Wizkid ni mmoja wa wanamuziki waliofanikiwa  kimuziki kwa kuitangaza vyema Afrika kwa kufanya kazi na wasanii wengi nje ya Afrika akiwemo Drake kutokea Marekani, Justine Skye na wengine wengi.

 Wizkid

Bila kumsahau msanii kutokea  Tanzania Diamond Platnumz ambaye anashika nafasi ya tatu kama msanii mwenye mashabiki millioni 4 kwenye kurasa yake ya instagram katika Bara la Afrika, huku Don Jazzy wa Nigeria akiwa nafasi ya 4 kutokea Nigeria kwa kuwa na masabiki million 3.4 na Peter wa PSquare kutokea Nigeria mwenye mashabiki million 3.
 Diamond Platnumz

 Don Jazzy
Peter wa Psquare

Saturday, September 30, 2017

NAY WA MITEGO AWATOLEA POVU WASANII WANAOTUMIA UCHAWI KATIAKA MUZIKI

Image result for nay wa mitegoMsanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego amefunguka juu ya wasanii wanaotumia uchawi katika muziki wao.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Makuzi’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa msanii akiamini katika ushirikina kuna kipindi kile anachokiamini kinaishiwa nguvu.

“Umefika muda karibia Tanzania nzima inaamini kwenye kile ambacho nakifanya, hii ni ndele tosha, ni zaidi ya ndele, sijua mtu ambaye anaamini hivyo” amesema Nay.

“Halafu ndele huwa zina mwisho ukifika muda maana wewe ndio umemaliza hata uimbe vipi, hata umshirikishe yesu bado watu hawaelewi” ameongeza.Katika hatua nyingine Nay amezungumzia uwezo wake katika performance jukwaani kwa kudai kuwa yeye Juma Nature wa pili kwani msanii huyo amekaa muda mrefu bila kutoa nyimbo ila bado anakubalika.

Image result for nay wa mitego

Tuesday, September 26, 2017

TAZAMA PICHA HIZI:MYWEATHER ANUNUA JUMBA LA BILIONI 56

 KWA watu wengi, kumiliki majumba Las Vegas na Miami ingetosha kuwafanya waone wameshamaliza kazi, lakini Floyd Mayweather yupo tofauti na wengi.

Bondia huyo Mmarekani ambaye hajawahi kupigwa katika pambano lolote kati ya mapambano yake 50 aliyocheza, anaendelea ku­furahia maisha ya kustaafu baada ya kumchapa Muiri­shi, Conor McGregor jijini Las Vegas.
Baada ya kumchapa McGregor katika raundi ya 10, inadaiwa Mayweather aliweka kibindoni zaidi ya pauni milioni 250 (Sh bil­ioni 752).
Bondia huyo ambaye amekuwa hajivungi ka­tika matumizi ya fedha na kufurahia jasho lake, amemwaga kitita cha pau­ni milioni 18.9 (zaidi ya Sh bilioni 56) kununua jumba kubwa la kifahari, katika eneo la watu wazito la Beverly Hills.
Kumbuka kuwa, Mayweather, 40, ana jumba jingine jijini Las Vegas, pia analo jingine Miami ambalo lina thamani ya pauni milioni 5.69 (zaidi ya Sh bilioni 17).
Jumba hili jipya alilonunua, lina vyumba sita vya kulala na mabafu kumi. Pia lina chumba maalu­mu cha sinema ambacho wanaweza kukaa watu 50 kwa raha kabisa, likiwa na mbwembwe nyingi zikiwemo mvinyo, bisi, chocolate na pipi.
Mayweather amecheza ngumi kwa miaka 21 na alistaafu Agosti 26 akiwa ameingiza fedha nyingi zaidi ya bondia yeyote yule kihistoria
Mmarekani huyo anadai kuwa yeye ndiye bondia wa kwanza kuingiza zaidi ya dola bilioni moja (zaidi ya Sh trilioni 2) katika mchezo huo mgumu zaidi.
Ukiachana na mkwanja aliotumia katika ku­nunua jumba hilo, inasemekana pia kuwa May­weather ametumia kiasi cha pauni 369,000 (zaidi ya Sh bilioni moja) kwa ajili ya kununua vitu vya ndani.












Friday, September 22, 2017

BAADA YA RAV 4,MABETTO KUSHUSHIWA PRADO MPYA?

Mwanamitindo ‘hot’ ambaye kwa sasa amegeuka mswaki kutokana na kuongelewa kila kona, Hamisa Mobetto, amewaacha watu njia panda baada ya kupost picha ya gari aina ya Prado yenye thamani ya zaidi ya milioni 50, mashabiki wanadai baada ya ile Rav 4, hiyo ni zawadi nyingine anatarajia kupewa na mzazi mwenziye ambaye ni Mbongo Fleva aliyezaa pia na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.



Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Mobetto aliposti picha ya gari hiyo na kuandika jina la mtoto wake.
“Dee Platnumz”

Kufuatia kauli ya Mobetto ya kudai kwamba yeye ndiye mwanamke pekee anayependwa na mwanamuziki huyo, mashabiki wakasema kwamba inawezekana ameagiziwa ndinga hiyo kwa ajili ya kumpeleka mtoto kliniki.

WEMA SEPETU ANASWA NA KIDUME KIPYA


Malkia wa Filamu za Bongo, Wema Sepetu amenaswa LIVE akiwa na mwanamme anayedaiwa kuwa ni bwana wake mpya. Wawili hao wamenaswa wakijiachia tena mchana kweupe peee huku Wema akijibebisha kwenye kifua cha jamaa huyo!
 
Anasikika Wema akitema madongo kumponda mpenzi wake wa zamani ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, kwamba alishamshauri aiboreshe perfume hiyo kama anataka iwe na viwango lakini mwenyewe akamwambia kwamba anataka aiuze kwa watu wa daraja la chini na kati.

Wednesday, September 20, 2017

BONDI JAKE LAMOTTA AFARIKI AKIWA NA MIAKA 95

Bondia wa zamani wa uzito wa kati na mchekeshaji Jake LaMotta,amefariki dunia akiwa na miaka 95, Mke wake amesema LaMotta amefariki nyumbani kwake kwa ugonjwa wa homa ya mapafu, Alikuwa mpiganaji maarufu zaidi miaka ya 40 na 50.



Atakumbukwa kwa uvaaji wa kaptula yenye mistari ya chuichui na wakati fulani alikua akiingiza uchekeshaji wakati akipigana jambo lililomfanya mpinzani wake kuishia kucheka na yeye kushinda.

Tuesday, September 19, 2017

HAMISA MABETO AMESEMA DIAMOND NDIYE BABA MTOTO WAKE

 Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameamua kuweka mambo hadharani kwa kumtaja baba wa toto wake wa pili AbdulLatif kuwa ni Diamond Platnumz.


Kwa mujibu wa akaunti ya mtandao wa Instagram ya mtoto huyo inaonyesha jina kamili la mtoto kuwa ni “Dully Dangote (AbdulLatif Naseeb Abdul Juma )Lion 🦁 (Leo) -8|8|2017 TanzanianBaby 👑 @hamisamobetto & Diamond Platnumz Son.”

Monday, September 18, 2017

WOLPER ASEMA MPENZI WAKE NI WA KIMATAIFA

Wolper akiwa na Mpenzi wake Brown

Muigizaji na mfanyabiashara wa mavazi nchini, Jacqueline Wolper amefunguka na kudai hatamani kumuona mpenzi wake akiendelea kufanya kazi zake za kimitindo ndani ya nchi kwa maana ameshaanza jitihada za kumtafutia kazi za kimataifa.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu Wolper amesema watu wanadai mpenzi wake ni mbeba pochi lakini anachojua ni wivu ndiyo unaowasumbua kwa sababu wanafahamu kazi anayofanya lakini kwa kuwa yeye anathamini kazi ya mpenzi wake huyo lazima atahakikisha anamvusha boda kwa kutumia mtandao alionao.

"Kuna mtu anamuita 'BFF' mbeba pochi, najua anafahamu ni kazi gani anafanya lakini kwa kuwa anaumia lazima amchafue. Mpenzi wangu ni 'model' ambaye ameshafanya kazi nyingi tu za kutembea majukwaani lakini si unajua sekta za mitindo hapa nyumbani?, hazijazingatiwa sana kwa hiyo mimi kwa kuwa tayari nina 'connection' nje nitampigania kuona anafanya kimataifa zaidi na siyo nyumbani" Wolper

Akizungumzia kuhusu mpenzi wake huyo kutumika kama mpendezeshaji video 'Video King' "Suala la kutumika kama 'video King' hapa nchini sitaki kabisa kusikia wala kuona kwa sababu hakuna maslahi, na mpaka sasa jiandaeni kuona 'suprise' kwani tayari kuna 'dea'l za kazi za South Afrika tumeshasaini mikataba kwa hiyo mambo ni mazuri upande wetu".

Mbali na hayo Wolper amesema haogopi kumsaidia mpenzi wake kwa hofu ya kuja kusalitiwa mbeleni kwani anaamini Mungu amempatia Brown kwa kuwa ana vigezo vyote anavyohitaji na hata ikitokea akamsaliti hatakuwa na shida kwani atakuwa daraja la mafanikio yake.

Saturday, September 16, 2017



Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee amefunguka na kusema kwa hali ilivyo sasa Tanzania ni wazi kuwa amani haipo kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma na kudai hali hiyo inaleta hofu miongoni mwa wananchi.

Lady Jaydee alisema  kitendo cha Mbunge Tundu Lissu pamoja na Meja Jenerali mstaafu wa JWTZ, Vincent Mritaba kupigwa risasi na watu wasiojulikana ni wazi kuwa amani ya nchi haipo.

"Ni kweli Tanzania hakuna amani kwa sababu kitendo cha mtu kupigwa risasi hadharani inatishia amani ukizingatia kuna wasanii wengine walikuwa wanatekwa unaogopa, sehemu yenye amani vitu kama hivyo haviwezi kutokea, na kitendo cha Meja mstaafu wa JWTZ kupigwa naye risasi inaongeza kabisaa Tanzani kuwa amani haipo naweza kuwa sina la kusema ila nikaishia kusikitika tu" alisema Lady Jaydee

Aidha Lady Jaydee anasema matukio haya yanaotoa picha mbaya kuwa kama nchi tunakokwenda si sehemu nzuri

GIGY MONEY AKATAA MAHARI YA MILIONI

Gift Stanford ‘Gigy Money’

 msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amejikuta akipishana na bahati baada ya kugomea mahari ya shilingi milioni 5 kutoka kwa mwanaume aliyetaka kumuoa.

Akizungumza  Gigy anayebamba na Wimbo wa Papa alisema, siyo kama hapendi kuolewa lakini anachoangalia ni thamani yake kwanza ambayo kama ni kutolewa mahari basi iwe zaidi ya milioni 5.

“Namshukuru Mungubahati ya kuolewa ninayo, lakini watu wanashindwa kutekeleza mahari yangu ninayotaka na sioni haja ya kukiuka kigezo changu sababu kama ridhiki ipo ipo tu.

“Kuna Jamaa alileta posa, lakini alivyopewa hilo sharti la milioni 10 jasho likamtoka, akalilia milioni 5 nikagoma, huo ndiyo msimamo ila uamuzi wa mwisho ni Muumba siwezi jua huenda kapuku akaniopoa huko mbeleni,”

Friday, September 15, 2017

DAIMOND AZIDI KUMPANDISHA PRESHA ZARI


Siku ya September 14, 2017 mpiga picha maarufu wa Diamond Platnumz, Kifesi alipost picha ya boss wake Diamond kwenye ukurasa wake wa instagram Picha ambayo alimpiga yeye, baada ya post hiyo mzazi mwenza na mpenzi wa Diamond Platnumz, Zari the Boss Lady akakoment kwenye post hiyo kwa kuweka emoji ya kidole cha kati.

Baada ya Zari kukomenti hivyo mashabiki wakahusisha hilo na swala ambalo Diamond anadaiwa ya kuwa yupo Zanzibar na mshindi wa Big Brother mwaka 2013 anayetokea Namibia, Dilish Methew huku ikisemekana wawili hao wanatoka kimapenzi kitu kilichomfanya Zari akomenti vile kwenye picha ya kifesi aliyompost Diamond.

Wednesday, September 13, 2017

HOSPITALI YA BUGANDO WAZUNGUMZIA HALI YA MC PILIPILI

Hali ya mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias maarufu Mc Pilipili aliyepata ajali ya gari bado haijaimarika, imeelezwa.


Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikolazwa Mc Pilipili, Lucy Joseph amesema yupo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu akisubiria kufanyiwa vipimo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amesema chanzo cha ajali ni mwendokasi.

Amesema ajali hiyo ilitokea jana Jumanne saa kumi jioni katika Barabara ya Mwanza – Shinyanga.

Haule amesema ndani ya gari aina ya Toyota Prado mali Mc Pilipili walikuwa watu watatu.

Kamanda Haule amesema dereva wa gari hilo alikuwa Saidi Hassan (28), mkazi wa Dar es Salaam na walikuwa wakitokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam.

Gari hilo amesema liliacha njia na kupinduka na kwamba, Mc Pilipili amepata majeraha sehemu mbalimbali mwilini ikiwemo kifuani.

Kamanda Haule amesema dereva alipata michubuko mkono wa kulia.

Katibu Muhtasi wa Kampuni ya Pilipili Events, Stella Maswenga alisema jana kuwa walipokea taarifa za ajali hiyo jana Jumanne jioni.

Maswenga alisema Mc Pilipili alialikwa mkoani Shinyanga kwa ajili ya kusherehesha harusi wikiendi iliyopita

BARNABA AFUNGUKA JINSI ANAVYO MMISI MAMA MTOTO WAKE

BURUDANI

Mwalimu na mwanamuziki wa bongo Fleva, Barnaba Elias 'Barnaba Classic' amefunguka na kudai anam-miss sana mama Steve 'Zuu Namela' japokuwa kwa sasa hayupo tayari kumrudia mzazi mwenzake huyo.

Msanii Barnaba akiwa na mama Steve 'Zuu Namela' enzi hizo mapenzi yakiwa moto moto kabla ya kuachana kwao.

Barnaba ameeleza hayo baada ya kupita muda mrefu tokea aachane na mzazi mwenzake huyo na kupelekea kuwa single mpaka kipindi hiki.

"Sitaweza kurudiana na mama watoto wangu japo nam-miss sana", amesema Barnaba.

Aidha, Barnaba amesema kwa upande wake mapenzi hayajawahi kumuendesha hata kidogo kama baadhi ya watu wengine wanavyokuwa baada ya kuachana na wapenzi wao kwa kushindwa hata kuendelea kufanya kazi zao.

"Niwe mkweli tu, mimi sijawahi kuendeshwa na mapenzi au mahusiano. Mapenzi hayana nafasi kubwa katika maisha yangu japokuwa yana nguvu kwa mtu yeyote yule, mapenzi hayajawahi kuchukua asilimia kubwa ya maisha yangu, kuniathiri wala kunitikisa", amesema Barnaba.

Pamoja na hayo, Barnaba ameendelea kwa kusema "Kila unachokiona kinatokea katika maisha yako kiwe kizuri au kibaya ni mapito tu, kwa sababu kilichotuleta duniani ni kingine na tunachokifanya ni kingine kwa hiyo muda mwingine kutendwa na vitu vingine ni kutenda dhambi zaidi 'so sometimes' unatakiwa upokee kwa furaha chochote utakachokumbana nacho katika maisha yako, kwa sababu hujui mpango wa Mungu ukoje. Ninachoamini mimi ni kwamba nilikuwa napita kwenye daraja ili niweze kuendela na safari aliyopanga Mungu 'so' sijui 'next' nilichopangiwa na Mwenyezi Mungu", amesisitiza Barnaba.

Kwa upande mwingine, Barnaba japo wameachana na Zuu lakini bado wanamawasiliano mazuri baina yao na kudai hivi karibuni aliongea naye kuulizia maendeleo ya Steve ya kimasomo na kumtumia pesa kwa ajili ya matumizi ya shule.

Tuesday, September 12, 2017

BILL NAS AKUNWA NA WATU WASIOJULIKANA

Bill Nas.

MKALI wa wimbo wa Sina Jambo, anayefahamika zaidi kwa jila la Bill Nas amefunguka kuwa hakuna kitu ambacho kinampagawisha kwa sasa kichwani kwake, kama matukio yanayofanywa na watu wasiojulikana.

 Bill Nas ambaye video ya wimbo wake huo mpya imetengenezewa Sauz na prodyuza Msafi ri alisema, mbali na kumpa pole Mwanasheria na Mbunge Tundu     Lissu wa tukio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana anatoa rai kwa jeshi la polisi ambao wanadhamana ya kusimamia usalama wa raia kuhakikisha wanakomesha matukio yanayofanywa na watu wasiojulikana.

“Kiukweli ukiwafi kiria watu wasiojulikana ni lazima upagawe.

Kwa sababu leo watu hao wamemfanyia unyama wa kutisha Lissu, ujui kesho uenda wakanifanyia mimi na wasichukuliwe hatua kwa sababu hawajulikani, kwa hiyo ifi ke hatua polisi wawafahamu hawa watu wasiojulikana!” Alisema Bill Nas

Monday, September 11, 2017

MFUMO WA ELIMU UNABAGUA WATU TANZANIA

Msanii Nikki wa Pili


Msanii Nikki wa Pili amedai kuwa watanzania wengi hawajapata elimu kutokana na kuwa mfumo wa elimu Tanzania unabagua watu na ndiyo maana hata wasanii wengi hawajaenda shule na siyo kwamba hawapendi shule.

Nikki amefunguka hayo na kusema kuwa mchakato wa michujo inayotumika kupata wasomi imekuwa ikiwatenga wanafunzi wenyewe na hali hiyo inasababishwa na elimu inayotolewa ili kumkuza mwanafunzi.

Nikki amesema kwamba licha ya kulalamikiwa wanafunzi wanalega shule ni kutokana na kukosa mfumo bora wa kuwapelekea wao kutimiza ndoto zao zaidi ya kukaririshwa kuhusu elimu.
"Nikienda shuleni sasa hivi nikimuambia mwalimu anipe wanafunzi 10 wenye akili ataniletea anayejua hesabu, physics na masomo mengine

NANDY AFUNGUKA BIFU LAKE NA RUBY

 Nandy.

MSANII wa Bongo, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema kuwa, japo watu wengi wamekuwa wakijadili kuhusu ukaribu wake na msanii wa zamani zao la Jumba la Kuibua Vipaji (THT), Ruby kwa madai kuwa kwa sasa hawapikiki chungu kimoja kutokana na ushindani uliopo baina yao, ishu hiyo si kweli kwani hana bifu na mwanadada huyo.
Ruby.

Nandy  anawashangaa wanavyosema hapatani na Ruby kwa madai kuwa anachukiwa kwa sababu amemfunika mwenzake kimuziki.

“Ukiniuliza mimi na Ruby nani anaimba vizuri, nitakujibu wote, yeye ana muziki wake nami nina wangu, sina ugomvi wala mazoea naye ila tukukutana tunasalimiana tu kama washikaji,” alisema.

Wednesday, September 6, 2017

KINGEREZA NOMA HAMORAPA KUJIFUNZA PRIVATE

Harmorapa.

BWA’MDOGO asiyekaukiwa matukio, Harmorapa anatarajia kuanza kujinoa katika suala zima la Lugha ya Kingereza kwa mtaalam wa kufundisha lugha hiyo, James Mramba ‘Mr. English’.

Hatua hiyo imekuja baada ya msanii huyo kuona kuna fursa anaikosa katika suala zima la kuwasiliana na wafanyabiashara mbalimbali hususan atakapokwenda kupiga shoo nje ya nchi.

“Nimeamua kujifunza Kingereza na sehemu sahihi kwangu ni kwa Mr. English kwa sababu anatoa huduma za mobile.

Atanifuata nyumbani, najifunza private,” alisema Harmorapa. 

Tuesday, September 5, 2017

MASOGANGE: NAJUTA KUWA STAA

Video queen mwenye umbo tata Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa, hakuna jambo analolijutia kama kuwa staa.

Masogange aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, alipokuwa hajulikani alikuwa akifanya vitu vyake kwa uhuru bila kutazamwa na mtu yeyote tofauti na sasa.

“Unajua mtu anaweza kusema ukiwa na jina unakuwa furaha sana, lakini si kweli kabisa, kuna wakati najuta huwa nakosa uhuru wa kufanya kitu chochote kama binadamu wa kawaida,” alisema Masogange mwenye umbo la kuvunja shingo za wanaume wakware.

LIL WAYNE ALAZWA HOSPITALI KWA KUUGUA KIFAFA

Mwanamuziki wa nyimbo za kufoka Lil Wayne

Mwanamuziki Lil Wayne amekimbizwa hospitalini baada ya kuanguka kutokana na kifafa na kupatikana akiwa hana fahamu katika chumba cha hoteli alimokuwa huko Chicago.

Mtandao wa wasanii wa TMZ umesema mwanamuziki huyo wa nyimbo za kufoka, 34, anayeugua ugonjwa wa kifafa, ameangushwa na ugonjwa huo mara kadhaa na alipoteza fahamu pindi tu alipowasili huko A&E.

Alitarajiwa kuwatumbuiza mashabiki wake huko Las Vegas siku ya Jumapili usiku.

Nyota huyo, ambaye kwa jina lake rasmi Dwayne Michael Carter Jr, alipokea matibabu mwaka uliopita baada ya kupoteza fahamu mara mbili lakini kwa kiasi kidogo.

Miaka minne iliyopita Lil Wayne alikuwa akipokea matibabu kwa siku kadhaa katika hospitali moja huko Los Angeles.

Baada ya kupata fahamu, mwanamuziki huyo aliambia kituo cha redio cha Power 106 kwamba, anaugua ugonjwa wa kifafa na yuko katika hatari za kukosa fahamu mara kadhaa.

Alimwambia DJ Felli Fel: ''Hiyo haikuwa mara yake ya kwanza, pili, tatu, nne , tano, sita au saba … nimepatwa na kifafa mara kadhaa, ni vile huwa hampati habari hizo.''

Lil Wayne amesema hupoteza fahamu baada ya kupatwa na msongo wa kiakili, kutopumzika na kufanya kazi kupita kiasi.

Mashabiki waliokuwa na wasiwasi wamekuwa wakituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kupitia #prayforweezy baada ya kisa cha mwanamuziki huyo kuripotiwa.

Mzaliwa huyo wa New Orleans, alianza taaluma hiyo akiwa na umri wa miaka 9, alipokuwa msanii mdogo kusajiliwa na rekodi ya Cash Money.

Tuzo zake tano bora za Grammy zinajumuisha tuzo ya albamu bora ya nyimbo za rap mwaka 2008 kwa albamu yake ya Tha Carter III na utumbuizaji bora wa rap kwa wimbo wake wa No Problem akiwa na Chance the Rapper & 2 Chainz.

Monday, September 4, 2017

CHID BENZ AMCHANA MADEE

Rapa Chid Benz ambaye kwa sasa amekuwa gumzo katika kila kona ya mitandao ya kijamii baada ya yeye kusema ana kolabo na 2pac, amefunguka kwa kumtolea povu Madee na kumwambia yeye ni mbea ndiyo maana haishi kumnanga kila kukicha.


Chid Benz ameeleza hayo kupitia kipindi cha 'Friday Night Live' (FNL), kinachorushwa na EATV pamoja na EA Radio baada ya siku kadhaa kupita tokea alipofanyiwa 'interview' na eNewz na kudai ana kolabo na 2pac, jambo ambalo watu wengi waliamini msanii huyo ameanza kuharibikiwa akili kutokana na dawa za kulevya na kupelekea Madee kutoa maoni yake binafsi kwa kudai ni bora yeye ambaye havuti hata sigara.

"Unaweza ukawa huvuti hata sigara lakini ukawa mbea, kwa sababu Madee watu tumnajua kama ni mbea na mnafki maana anapenda kuninanga, anahisi labda mimi ipo siku nitafanya kitu", alisema Chid Benz.

Pamoja na hayo Chid Benz aliendelea kwa kusema "mtu kama anaku-post kitu katika mitandao ya kijamii halafu chini yake anakuandikia 'ndiyo maana mimi sivuti hata sigara' 'that means' anaonyeshea watu kwamba kuna kitu Chid Benz anatumia au anavuta ndiyo maana yeye hatumii sigara kwa hiyo mimi amenitengenezea ubaya mpaka kupelekea watu ku-comment kwamba madawa yamenisababisha nichanganikiwe", alisisitiza Chid Benz