Tuesday, February 20, 2018

MWILI WA MWANAFUNZI AKWILINA KUAGWA ALHAMISI NIT DAR

Msemaji wa Familia ya Akwilina, Festo Stephen amesema mwili wa binti yao unatarajiwa kuagwa siku ya Alhamisi katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) endapo watapewa ruhusa hiyo na chuo, kama itashindikana watamuaga katika Kanisa la Mbezi Luis

Festo amebainisha hayo baada ya watu wengi waliopo jijini Dar es Salaam kutaka kufahamu ratiba nzima ya mazishi za binti huyo zitafanyika wapi ili waweze kuenda kutoa heshima zao za mwisho wa marehemu kabla ya kupelekwa katika nyumba yake ya milele.

"Mwili wa marehemu utaagwa Alhamisi katika Chuo cha NIT endapo tutajibiwa maombi yetu au katika Kanisa la Mbezi Luis na siku ya Ijumaa atazikwa Mashati Wilayani Rombo katika kijiji cha Marangu Mkoani Moshi ambako wapo wazazi wake", amesema Festo.

Mnamo Februari 16, 2018 Akwilina alipigwa risasi akiwa kwenye daladala ambayo inasemekana ilikuwa inapita eneo ambalo polisi walikuwa wakiwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakielekea kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Kinondoni.

No comments:

Post a Comment