Mtuhumiwa wa utekaji watoto Arusha, Samson Peter amefariki kwa kupigwa risasi akijaribu kuwakimbia polisi, leo jijini Arusha.
Samson Peter alikamatwa usiku wa tarehe 2, mwezi huu baada ya timu maalumu ya Polisi ya askari tisa, watano kutoka Arusha wakiongozwa na Mkaguzi wa Polisi Amani na wa Geita askari wanne wakiongozwa na Mkaguzi wa Polisi, James, kuizingira nyumba ya wageni aliyokuwa amejificha mtuhumiwa na mtoto aliyemteka tangu Septemba Mosi.
No comments:
Post a Comment