Siri
imefichuka, kumbe Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimpunguzia
mshahara aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa, mbaya zaidi
hata huo waliokubaliana TFF ilishindwa kumlipa na sasa kocha huyo
anataka kwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ili kushinikiza
alipwe deni lake.
Mkwasa
ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Yanga, alipewa jukumu la kuinoa Taifa
Stars baada ya kutimuliwa kwa Mart Nooij raia wa Uholanzi ambaye
alikuwa akilipwa Sh milioni 28 kwa mwezi.
Mkwasa
alisema wakati akiinoa Taifa Stars alikubaliana na TFF kupunguza
mshahara wake lakini hata baada ya kufanya hivyo, shirikisho hilo
lilishindwa kumlipa na kujikuta likiweka deni la Sh milioni 80 hadi
sasa.
“Hadi
sasa sijalipwa fedha yoyote na TFF katika kile kiasi ninachodai, kwanza
nilipunguza mshahara kwa makubaliano nao lakini hata huo tuliopunguza
hawakunilipa na kuweka deni hilo.
“Kama
hali ikiendelea kuwa hivi, nitapeleka malalamiko yangu Fifa ili nilipwe
haki zangu kwa maana naona hakuna dalili za kulipwa licha ya kuweka
mikakati kadhaa ya kunilipa ikiwemo kulipwa nusu kwanza.
“Kwa
sasa naendelea kuwasikilizia nione lini watanilipa, kama wakiendelea
kukaa kimya basi nitaenda kuwashtaki Fifa ili haki yangu niipate
haraka,” alisema Mkwasa.
No comments:
Post a Comment