.

.
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Tuesday, October 10, 2017

KOCHA ALIMWA KADI NYEKUNDU KWA KUZURURA OVYO UWANJANI

Kilimanjaro. Mchezo wa SDL kati ya AFC Arusha na Pepsi zote za Arusha uliochezwa Jumatatu katika Uwanja wa Ushirika na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, umeibua malalamiko baada  ya mwamuzi wa kati kudaiwa kuharibu mchezo huo, huku kocha wa AFC akilimwa kadi nyekundu.

Mwamuzi Goodluck Simba kutoka Pwani alilaumiwa na AFC kuwa aliwapa Pepsi bao ambalo sio halali pamoja na kuwanyima penalti, katika mchezo huo kocha mkuu wa timu ya AFC, Gerald Totoo alioneshwa kadi nyekundu kwa kuondoka eneo lake wakati mchezo ukiendelea.
Totoo alisema baada ya kurudi katika eneo lake alishangaa kuoneshwa kadi nyekundu wakati hakufanya jambo lolote baya kwa mwamuzi wala kwa kamisaa wa mchezo huo
“Baada ya kuona mwamuzi anachezesha sivyo nilimfuata kamisaa wa mchezo huo Babtise Mihafu aliyekuwa jukwaani na kumweleza jinsi ataharibu mchezo, kisha nikarejea kwenye benchi langu,” alisema Totoo.
 Kocha huyo aliongeza kuwa, timu zinapaswa kuwa makini kwa kila mchezo hasa za Arusha ambazo zimehamia Moshi kwenye Uwanja wa Ushirika wasipokuwa makini itawagharimu.

Monday, October 9, 2017

NENO LA DROGBA KWA SALAH

Image result for PICHA YA DROGBA

Nyota wa zamani wa Ivory Coast na Chelsea Didie Drogba amempongeza winga wa Liverpool na Misri  Mohamed Salah baada ya kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

Salah alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa Kundi E kuwania kufuzu kombe la dunia kutoka Afrika dhidi ya DR Congo jana usiku.

Drogba ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kumpongeza Salah ambapo ameandika, “Hongera kaka yangu, Najivunia wewe, umekuwa kiongozi bora kwenye taifa lako, umenikumbusha mimi na Ivory Coast mwaka 2006”.

Baada ya ushindi wa jana Misri, imefikisha alama 12 na kufanya iwe timu ya pili kufuzu kombe la dunia 2018 kutoka Afrika baada ya Nigeria.

Hii ni mara ya kwanza kwa Misri kufuzu fainali za Kombe la dunia baada ya miaka 28 kupita ambapo mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 1990 wakati huo Mohamed Salah hajazaliwa.

NIGERIA YAIONGOZA AFRIKA KUINGIA KOMBE LA DUNIA

Timu ya Taifa ya Nigeria imekuwa ya kwanza kutoka barani Afrika kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi baada ya kufanya vyema kwenye michezo yake.

Katika ushiriki wao mara 6 kwenye Kombe la Dunia tangu mwaka 1994, 1998 na 2014 waliishia raundi ya pili, huku mwaka 2002 na 2010 waliishia hatua ya makundi.

Taifa jingine lililojikatia tiketi hiyo mapema ni Costa Rica ikiwa ni mara yao ya tano kushiriki Kombe la Dunia.

Friday, October 6, 2017

UJERUMANI YAFUZU KWA KOMBE LA DUNIA 2018

Germany walihitaji kutoka sare au kushinda kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018

Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Ujerumani wamefuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Urusi baada ya kulaza Ireland Kaskazini 3-1 mjini Belfast.
Sebastian Rudy alifunga bao dakika ya pili, Sandro Wagner akaongeza la pili baadaye, naye Joshua Kimmich akafunga la tatu mechi ikikaribia kumalizika.
Josh Magennis alifungia Ireland Kaskazini bao la kufutia machozi kwa kutumia kichwa dakika za lala salama.
Ujerumani wamefuzu wakiwa viongozi wa kundi lakini Ireland Kaskazini wanasalia bado na matumaini ya kufuzu kupitia mechi za muondoano za kufuzu Novemba.
Vijana hao wa Michael O'Neill watamaliza mechi zao Kundi C nchini Norway Jumapili, wakilenga kumaliza wakiwa miongoni mwa timu nane bora zitakazomaliza nafasi ya pili kati ya makundi tisa ya kufuzu.
Ireland Kaskazini wameshindwa mechi zao mbili kundini mikononi mwa Ujerumani

Thursday, October 5, 2017

OMOG ATOBOA SIRI YA USHINDI

KOCHA MKUU WA SIMBA, JOSEPH OMOG.

Ndoto ya kutaka kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania ni moja ya sababu zinazowafanya wachezaji wa Simba kucheza kwa bidii na juhudi katika kila mechi ya Ligi Kuu Bara, hayo ni maneno ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog.
Akizungumza na gazeti hili jana mchana, Omog, aliitaja sababu nyingine ni "kiu" ya kukosa ubingwa katika misimu minne mfululizo, hivyo kuwafanya wachezaji walioko katika kikosi hicho kupambana ili kuhakikisha wanalipa deni linalowakabili.
"Kila mchezaji, kiongozi na shabiki wa Simba anafikiria ubingwa wa ligi, wote tunafahamu tunahitaji kuhakikisha furaha hii inapatikana, tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha haturudii makosa yaliyotokea msimu uliopita," alisema Mcameroon huyo.
Aliongeza kuwa ushindani ambao wanakutana nao unawasaidia kuwaimarisha wachezaji wake na kujiweka tayari na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika na nafasi ya kutetea Kombe la FA.
"Hakuna mchezaji mwenye namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza, kila mchezaji anatakiwa kupambana ili apate nafasi, tuna wachezaji zaidi ya 20, lakini anayefanya vizuri na aliye "fiti" ndiye ataingia katika kikosi cha kwanza na wengine watasubiri, huo ndiyo utaratibu wa kusaka ushindi," Omog alisema.
Alieleza pia anawakumbusha wachezaji wake kutodharau timu yoyote inayoshiriki ligi hiyo kwa sababu ili malengo yao yatimie ni lazima wasipoteze mchezo wowote iwe nyumbani au ugenini.
Simba wenye pointi 11 sawa na Mtibwa Sugar na Azam FC, ndiyo vinara wa ligi hiyo na mchezo wao unaofuata utakuwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa Oktoba 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

SIMBA WAIFUNGUKIA CCM

Baada ya Simba kushinda kwa bao 1-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Dodoma FC, klabu hiyo imekiomba chama tawala cha CCM kufanya ukarabati katika viwanja inavyovimiliki.

Simba ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Said Ndemla nje ya 18 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema mechi ilikuwa nzuri lakini uwanja ulikuwa tatizo kubwa.
“Mechi ilikuwa nzuri na timu yetu ilicheza vizuri, Dodoma FC pia walicheza vizuri.
“Lakini nikiombe Chama cha Mapinduzi kufanya ukarabati katika viwanja vyake ili kurahisisha uchezaji,” alisema.
Simba imecheza mfululizo katika viwanja vinne vyote vinavyomilikiwa na CCM na vitatu kati yake vilikuwa dhoofu el hali.
Mechi ya kwanza ilikuwa dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambao ulionekana ni wenye nafuu. Baada ya hapo ikasafiri hadi Tabora kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Milambo. Mechi ilichezwa kwenye Uwanja wa CCM na uwanja ulikuwa hoi.
Mechi ya tatu Simba walicheza na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage ambao ulikuwa dhoofu kwelikweli na baada ya hapo walisafiri hadi Dodoma kucheza mechi hiyo ya kirafiki kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Wednesday, October 4, 2017

HUU NDIO UAMUZI WA SIMBA

Benchi la ufundi la Simba limefunguka kuwa baada ya kukwaa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa sasa hawatakubali kung’oka kwenye nafasi hiyo hadi mwisho wa ligi ambapo watatwaa ubingwa kwa msimu huu.

Simba chini ya bosi wao mkuu, Joseph Omog walifanikiwa kurejea kileleni mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stand United, na kufikisha pointi 11 wakiwa sambamba na Mtibwa Sugar na Azam, lakini wao wanaongoza kwa idadi ya mabao ya kufunga.
Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema kuwa kwa muda mrefu walikuwa wanawaza kukalia usukani wa ligi ambapo baada ya sasa kupata nafasi hiyo watahakikisha wanashinda kwenye kila mchezo wao kwa ajili ya kuendelea kukaa kwenye nafasi hiyo na hawana mpango wa kushuka.
“Kiukweli tulikuwa tunataka tuwepo hapa tulipofika kwa sasa, yaani kuziongoza timu nyingine na hilo kwa sasa tumeshalifanikisha na tunachokipanga kwa sasa ni mbinu za kushinda kwenye kila mchezo wetu ujao.
“Ujue wakati tulipokuwa chini, mashabiki hawakuwa wanaelewa kwa sababu wanaona tuna kikosi imara kuliko hata wapinzani wetu wengine, lakini kwa sasa presha imepungua na tunaweza kufanya vizuri kwenye kila mchezo wetu kwa sababu tunacheza tukiwa na akili moja ya kushinda hapa ndiyo basi hatushuki tena,”alisema Mayanja.

SOURCE: CHAMPIONI

ARSENE WENGER APATWA NA HOFU KUHUSU BARCELONA KUHAMIA EPL

Masuala ya kisiasa yanayoendelea nchini Hispania tayari yameleta habari nyingi za kisoka, lakini kubwa ni uwezekano wa vilabu vya Catalunya kuhamia katika ligi zingine ikiwemo Epl.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaonekana kutofurahia habari za Barcelona kuhamia katika ligi kuu ya Uingereza huku akihoji Barcelona watahamiaje wakati kuna vilabu vya Scotland havijahamia hadi leo.
Wenger amesema haitakuwa sahihi kwa FA kuruhusu jambo hilo kutokea huku wakivikatalia vilabu vya nchi jirani ya Scotland kuhamia katika ligi hiyo.
Sii hivyo tu lakini mzee Wenger ameonya kuhusu mbio za ubingwa wa Epl kwamba zinaweza kuwa ngumu mno kama miamba hiyo ya La Liga itapewa ruhusa kujiunga na ligi kuu Uingereza.
Wiki iliyopita waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Hispania alisema vilabu vya Catalunya vinaweza kuhamia katika ligi za jirani endapo Catalunya watapata uhuru wao.

Tuesday, October 3, 2017

NEYMAR AUMIA KIDOLE

Brazil inajiandaa kuivaa Bolivia na Chile katika mechi za kuwania kucheza Kombe la Dunia, Hata hivyo, Brazil wameishafuzu.
Imeelezwa Neymar anayechezea PSG ya Ufaransa ameumia lakini si kwa kiwango kikubwa cha maumivu.

KIKOSI CHA TAIFA KUANZA MAZOEZI KESHO,KWA AJILI YA JUMAMOSI

Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinatarajiwa kuanza mazoezi kesho asubuhi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, eneo la Bunju mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi Jumamosi ijayo.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas ameiambia Bin ameeleza kuwa kikosi hicho kitafanya mazoezi kwenye Uwanja huo kwa siku tatu kabla ya kuhamia Uwanja wa Uhuru.
Tayari Msuva, mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga yupo nchini, wakati Samatta mchezaji wa zamani wa Simba SC anatarajiwa kuwasili usiku wa leo.
Kwa ujumla kikosi kiliochoteuliwa na kocha Salum Shaaban Mayanga kwa ajili ya mchezo huo kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).
Mabeki Gardiel Michael (Yanga), Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (BarokaFC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar).

Viungo ni Himid Mao ambaye pia ni Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Yanga), Simon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Ibrahim Hajib (Yanga) na Mbaraka Yussuph (Azam FC). 

Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Ame Ninje (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).  

ALVARO MORATA:MSHAMBULIAJI WA CHELSEA APATA JERAHA

Alvaro Morata
Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata huenda akakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya kupata jeraha la misuli ya paja wakati wa mechi ambayo walilazwa 1-0 na Manchester City Jumapili.
Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 24 alijiunga na Chelsea kwa £60m majira ya joto kutoka Real Madrid, ada iliyovunja rekodi Chelsea.
Amewafungia Blues mabao saba kufikia sasa.Madaktari wa timu ya taifa ya Uhispania wanasema alipata jeraha la ngazi ya tatu kwenye misuli yake ya paka na hataweza kuwachezea mechi za kufuzu za Kombe la Dunia dhidi ya Albania na Israel wiki hii.
Majeraha kama hayo kwenye misuli mara nyingi huchukua wiki nne hadi nane kupona.Uhispania wanaongoza Kundi G wakiwa alama tatu mbele ya Italia, wakiwa wamesalia na mechi mbili.Alvaro MorataChelsea wamepangiwa kucheza dhidi ya Crystal Palace 14 Oktoba na baadaye dhidi ya Roma, Watford na Everton.

TAARIFA KUHUSU MAENDELEO YA DONALD NGOMA

Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma jana hakufanya mazoezi pamoja na wachezaji wengine kutokana na majeraha ya msuli aliyoyapata siku ya mechi ya Jumamosi wakati Yanga ilipocheza dhidi ya Mtibwa Sugar.Ngoma alipewa saa 24 hadi 48 za uangalizi chini ya daktari wa Yanga ili kuona maendeleo kabla ya kutoa majibu kama anaweza kurudi uwanjani mapema au vinginevyo.

Leo asubuhi ShaffihDauda.co.tz imezungumza na Godlisten Chicharito ambaye yupo kwenye timu ya kitengo cha habari ndani ya Yanga ambapo amesema, hali ya Ngoma inaendelea kuimarika.

“Jana hakufanya mazoezi alikuwa chini ya uangalizi wa daktari kuona maendeleo ya jeraha lake. Lakini kwa sasa anatembea vizuri ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo, anaweza kufanya mazoezi binafsi ikiwa ni tiba ya jeraha lake”-Chicharito.

Yanga inakabiliwa na mchezo wa VPL dhidi ya Kagera Sugar October 14, 2017 kwenye uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.

Sunday, October 1, 2017

WACHEZAJI WA SOKA WAMPINGA TRUMP MAREKANI

Wachezaji wakiwa wamegoma kwa namna tofauti
Wachezaji wa ligi ya soka Marekani kwa pamoja wameendelea kumpinga Rais Trump kwa kugoma kuimba wimbo wa Taifa la nchi hiyo katika mchezo wa Jumapili.
Walionekana wakiwa wameweka tu mikono vifuani ama mabegani mwa wachezaji wenzao huku wimbo huo ukiendelea.
Wengine walipiga magoti.
Cam Newton mchezaji nyota wa Carolina Panthers yeye alinyoosha mkono wake juu wakati wimbo huo ukiimbwaBado haijajulikana ni lini itakuwa mwisho wa mgomo huuHata hivyo mgomo wa wiki hii haukuwa na nguvu kama wa wiki iliyopita.
Katika mchezo baina ya Dallas Cowboys na Los Angeles Rams uliendelea bila ya mgomo wowote.
Trump ameandika katika mtandao wa Tweeter akiwataka viongozi wa chama cha soka Marekani kuwachukulia hatua wote waliohusika.
Mgomo huo ulianza mwaka jana baada ya mchezaji Colin Kaepernick wa San Francisco 49ers kuelezea namna raia weusi wa Marekani wanavyoteseka baada ya mlolongo wa kupigwa risasi na polisi.

Saturday, September 30, 2017

Dele Alli apigwa marufuku kwa kuonyesha ishara ya kidole cha kati

Dele Alli apigwa marufuku kwa kuonyesha ishara ya kidole cha kati
Kiungo wa kati wa Uingereza Dele Alli amepigwa marufuku kutoshiriki mechi moja ya kimataifa kufuatia hatua yake ya kuinua kidole cha kati wakati wa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Slovenia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atashiriki mechi dhidi ya Lithuania siku ya Jumapili.
Alli alisema kuwa ishara hiyo ilimlenga aliyekuwa mchezaji mwenza wa Spurs Kyle Walker wakati wa dakika ya 77 ya udhindi wa 2-1 katika kundi F.
Kisa hicho kilitokea baada ya Alli kupigwa kumbo na beki wa Slovakia Martin Skrtel huku refa Clement Turpin akionyesha ishara ya mchezo uendelee.
Ilionekana kana kwamba Alli alimuonyesha ishara hiyo ya kidole cha kati afisa huyo ambaye pia walirushiana maneno alipotolewa  dakika ya 93.

Friday, September 29, 2017

WANAWAKE WA TANZANIA KUKABILIANA NA NIGERIA

Tanzania
Timu ya soka ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ya Nigeria inatarajiwa kutua jijini Dar es salaam leo ijumaa ikiwa na kikosi cha watu 31 .
Timu hiyo inataraji kucheza na Tanzania 'Tanzanite' mchezo wa marudiano kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Ufaransa .
Mchezo huo utafanyika Jumapili Oktoba mosi Uwanja wa Chamazi nje ya jiji la Dar es Salaam, Mchezo wa Awali Tanzania ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 nchini Nigeria.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewapa fursa mashabiki wengi kuingia uwanjani kuishangilia timu yao ya taifa The Tanzanite.

ARSENAL YANAWIRI-EUROPA LIGI

Arsenal
Michuano ya Uefa Europa Ligi imepigwa usiku wa kuamkia leo kwa michezo mbalimbali hatua ya Makundi.
Klabu ya Arsenal ikiwa ugenini Imeshinda mabao 4-2 dhidi ya Bate Borisov, Everton imetoka sare ya bao 2-2 na Apollon, Ac Millan imeshinda 3-2 dhidi ya Rijea, Lyon pia wamefanikiwa kutoa sare na Atlanta baada ya kufungana bao 1-1.
Nice imeichapa Vitese mabao 3-0, Mainz imefungwa bao 1-0 na Hoffeinheim, Partizan imechapwa na Dynamo magoli 3-2 na Maccab Tel Aviv imetoka sare na Villareal 0-0.
Fc sheriff imetoshana nguvu na Koeben kwa sare ya kutofungana 0-0, Lugan imeambulia kipigo cha bao 2-1 dhidi ya FC FCSB ,Plesen imeichakaza Hapoel bao 3-0.
FC Cologne imefungwa bao 1-0 na FK Crvena Zvezda, Salzburg imeshinda bao 1-0 dhidi ya Marseille, Oestersunds FK imeichapa Hertha Berlin bao 1-0, Konyaspor imetakata kwa ushindi wa bao 2-1 na Vitoria de Guimaraes.
AEK Athens imetoshana nguvu na Austria Wien ya bao kwa kufungana bao 2-2

Thursday, September 28, 2017

SIMBA NA YANGA WAZUA GUMZO

Gumzo la mechi ya watani Yanga na Simba itakayochezwa Oktoba 28 limezidi kupanda baada ya kuelezwa kuwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, utakuwa katika matengenezo.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema jana, uwanja huo unahitaji muda wa miezi mitatu zaidi na akaahidi utakuwa bomba ile mbaya.Tayari kampuni ya kubashiri ya SportPesa imeanza kufanya ukarabati katika uwanja huo.

Lakini taarifa hiyo, kwamba hadi Oktoba 28 uwanja utakuwa katika matengenezo inaonekana kuwashitua mashabiki wengi.
Tayari kumezuka mijadala kuhusiana na wapi watani hao watacheza mechi yao hiyo.
Mashabiki wengi wangependa kuona timu hizo zinacheza kwenye uwanja huo kama ilivyozoeleka.
Wengi wamekuwa wakihoji kama Uwanja wa Uhuru unaweza kuibeba mechi hiyo ana wengine wameshauri mechi ihamishiwe CCM Kirumba, Mwanza.
Lakini wako wanatania kuwa hata Chamazi itatosha na wamekuwa wakishambuliwa kuwa hawako makini katika jambo muhimu.
Bado halijawa tamko rasmi au Yanga na Simba hazijapata barua baada ya maneno ya waziri, huenda zikajadiliana na kutangaza wapi zingependa kwenda.

ARSENAL WAGENI WA BATE BORISOV-EUROPA LEUROPE

Arsenal wageni wa BATE BorisovMichuano ya Uefa Europa League inatarajiwa kuchezwa hii Leo kwa michezo kadhaa ikiwa ni hatua ya Makundi, miongoni mwa michezo ambayo inatazamiwa kuchezwa BATE Borisov wanacheza na Arsenal, Salzburg dhidi ya Marseille, Zenit wanawakaribisha Sociedad, Everton ni wenyeji wa Apollon, Locomotiv watakuwa ni wenyeji wa Fastav, Maccabi Tella Viv wanawaalika Vilareal , Lyon inamenyana na Atalanta .Arsene Wenger  FC Astana ni wenyeji wa Slavia Prague, Partizan Beograd wanawaalika Dynamo Kyiv, Skenderbeu ni wenyeji wa Young Boys, FC Cologne watamenyana na FK Crvena Zvezda, AC Milan ni wenyeji wa Rijeka.

LWANDAMINA:MTIBWA NI "PASUA KICHWA"

GEORGE LWANDAMINA.
Kocha wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, George Lwandamina, amesema kuwa mechi dhidi ya Mtibwa Sugar itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Uhuru "si ndogo" kama ambavyo baadhi ya wadau wanavyoiangalia.
Akizungumza Lwandamina, alisema kuwa matokeo mazuri waliyonayo Mtibwa Sugar yanawasaidia kuondoa wasiwasi katika mechi itakayowakutanisha na hivyo anaamini itakuwa na changamoto zaidi kwa upande wake.
Lwandamina alisema kuwa anaamini uzoefu wa mechi za kimataifa na faida ya kucheza nyumbani ndiyo vitu anavyovitegemea kumsaidia kupata ushindi katika mchezo huo.
"Mechi dhidi ya Mtibwa Sugar ni ngumu na ya ushindani, ni moja kati ya klabu zenye wachezaji wanaojua kupambana," Lwandamina alisema kwa kifupi.
Kocha huyo wa zamani wa Zesco ya Zambia aliongeza kuwa anaamini wachezaji wake watapambana, ili wapate pointi zote tatu katika mechi hiyo na kukaa katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.
Mzambia huyo alifurahi kuona mshambuliaji wake wa kimataifa, Amissi Tambwe, anaendelea vyema na uamuzi wa kumpanga utajulikana kesho baada ya kumaliza mazoezi.