Mahindi yaliyoibiwa, imeelezwa, ni mali ya Mariam Joseph na kwamba kundi hilo lilivunja mlango wa nyumba yalimokuwa yamehifadhiwa mahindi hayo usiku katika kata ya Buahalahala wilaya na mkoa wa Geita.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Mponjoli Rodson alisema uchunguzi unaendelea na kwamba majina ya marehemu hayajafahamika.
Mtu wa nne ambaye alinusurika kuuawa na mwili wake kuchomwa moto baada ya kuokolewa na polisi ametajwa na Kamanda Rodson kuwa ni Matokeo Malomo (20).
Habari kutoka Mtaa wa Mwatulole kulikofanyika mauaji hayo zilidai kuwa wananchi walitumia fimbo na mawe kuwashambulia watuhumiwa hadi kifo.
Habari hizo zilieleza zaidi kuwa baada ya kufariki, mmoja wa wananchi hao alichoma moto miili ya watu hao.
Habari hizo kutoka chanzo cha kuaminika zilieleza zaidi kuwa mtu wa nne aliyekuwa na marehemu aliokolewa na polisi waliofika eneo la tukio la wizi, ingawa hakikuweza kufafanua zaidi 'bahati' hiyo.
Kamanda Mponjoli alisema watu kadhaa wanashikiliwa kwa mauaji hayo baada ya kukamatwa juzi asubuhi, lakini hakuweza kutaja idadi wala majina yao mara moja.
Kumekuwapo kwa uhaba na bei ghali ya chakula katika maeneo mengi ya nchi, mkoa wa Geita ukiwa mmojawapo.
Uchunguzi wa Nipashe unaonyesha hali hiyo imetokana na ukame wa muda mrefu ambao ulisababisha mazao kukauka.
Gunia moja la mahindi (sawa na debe sita) linauzwa kwa bei ya wastani wa Sh. 112,000 kwa sasa, uchunguzi wa Nipashe umeonyesha.
SH. 65,000
Matukio ya watu kuuwawa na kisha kuchomwa moto mkoani Geita yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara tangu wanaume watano kuuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kuchomwa moto kwa tuhuma ya kuiba Sh. 65,000 za rambi rambi Desemba 2013.
Marehemu hao walishambuliwa wakiwa mikononi mwa walinzi wa jadi (sungusungu).
Watu hao walidaiwa kuiba mchango usiku nyumbani kwa John Ibarabara baada ya kuvamia nyumba ya mfiwa ikiwa ni siku moja baada ya ndugu, marafiki na majirani, wakiwemo watuhumiwa kutawanyika.
Ilidaiwa kuwa marehemu hao walirudi nyumbani kwa mfiwa usiku na kuvunja mlango na kutaka wapatiwe fedha ya rambirambi.kufanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa akiwa na damu kwenye nguo zake na walipomhoji aliwataja watu wengine ambao walikamatwa wote.

No comments:
Post a Comment