Friday, June 1, 2018

YANGA YAZICHANA KLABU ZINAZOSAJILI KUPITIA MLANGO WA UWANI


Wakati vuguvugu la usajili wa awali likiendelea kuteka vichwa vya wadau wa soka nchini, uongozi wa Yanga umefunguka kuhusiana na baadhi ya klabu zinazosajili kupitia mlango wa uwani.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kuwa kuna baadhi ya klabu 'hajazitaja' zimekuwa zikisajili wachezaji pale wao wanapowataja.

Kutokana na vitendo hivyo kusubiri Yanga itaje wachezaji ilio kwenye mipango nao kisha timu zingine zinaibuka na kuwasajili, Mkwasa amesema kuwa huo ni usajili wa uwani unaoonesha mapungufu kwa wapinzani.

Mkwasa amefunguka kwa kusema kuwa hilo linaonesha kuwa namna gani Yanga ina kiwango kikubwa cha kuchagua wachezaji tofauti na klabu zingine ambazo zimekuwa zikisubiri wataje majina kisha ziwakimbilie kuwachukua.

"Unajua kuna klabu zimekuwa zikisubiri sisi tutaje majina kisha zikimbilie kuwasajili, hilo linaonesha namna gani sisi tunakuwa na uwezo mkubwa wa kuuchagua wachezaji tofauti na wanaowasajili kupitia mlango wa uwani" amesema Mkwasa.

No comments:

Post a Comment