Askari
hao watakuwa wakilinda usalama wa ndani na nje ya uwanja huo uliopo
Manispaa ya Temeke na mtu yeyote atakayefanya fujo au uharibifu ataishia
mikononi mwao.
Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema,
askari hao watashirikiana na watu wengine kutoka majeshi mengine na
kampuni binafsi za ulinzi kuhakikisha usalama unatawala uwanjani hapo.
“Kuna
polisi 350 ambao leo (jana) jioni watafanya mazoezi uwanjani
wakijipanga kwa ajili ya kulinda kesho (leo) kuhakikisha hakuna vurugu
au uhalifu wowote utakaotokea.
“Nawasihi
wote watakaofika uwanjani kutazama mechi kwa utulivu na kutofuata
mkumbo wa kufanya fujo kwani wataishia mikononi mwa polisi na walinzi
wengine wa siri.
“Hatuwezi
kukubali kuona watu wanajipanga kuharibu miundombinu ya uwanja ambao
tulipata tabu kuomba uruhusiwe kwa timu hizi, nawasihi watu wasifanye
vurugu,” alisema Lucas.
No comments:
Post a Comment