Wednesday, March 22, 2017

UFARANSA: WAZIRI AJIUZULU


Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa,Bruno Le Roux, amejiuzulu, baada ya kuibuka shutuma kuwa aliwaajiri binti zake wawili kuwa wasaidizi wa bunge wakiwa wanafunzi.

Waendesha mashtaka walifanya uchunguzi wa awali kuhusu mikataba yenye thamani ya karibu dola elfu sitini ambazo bwana Le Roux aliwapa binti zake kati ya mwaka 2009 na mwaka 2016.

Amesema hakuna sheria ya bunge iliyokiukwa na watoto wake walifanya kazi kwa uhalali, lakini hakutaka kuwa kikwazo kwa Serikali.

Wakati huohuo, uchunguzi kama huo umeendelea kufanyika dhidi ya mgombea urais kutoka chama cha Conservative Francois Fillon, ambaye anashutumiwa kufanya udanganyifu.

Fillon amekana kuajiri familia yake na kuwalipa mishahara minono, kashfa ambayo imetia dosari mchakato wake wa kuwania urais

No comments:

Post a Comment