Huku
wakiwa wanajiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco
ya Zambia, uongozi wa Yanga umesema wala hawana hofu huku ukipanga
kuwatumia Obrey Chirwa na Justine Zullu wanaotoka nchi moja na wapinzani
wao.
Kauli
hiyo, ameitoa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa baada ya wapinzani
wao kutotoa taarifa za ujio zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya pambano
hilo.
Timu
hizo, zinatarajiwa kuvaana Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana wiki moja ijayo huko Lusaka,
Zambia.
Mkwasa
amesema huo usiri wanaoufanya Zanaco wala hawauhofii, kwani timu yao
ina wachezaji na makocha, George Lwandamina na Noel Mwandila waliokuwa
wanaifundisha Zesco inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia.
Mkwasa
alisema, anaamini kabisa kwa kupitia wachezaji wao, Chirwa na Zullu
watazipata mbinu wanazozitumia wapinzani wao katika mechi hiyo.
Aliongeza
kuwa, hadi hivi sasa hawajapata taarifa ya ujio wao kama watawalipia au
kujilipia wao hoteli na huduma nyingine mara watakapotua nchini.
"Niseme
tu kuwa, hadi hivi sasa uongozi wa Yanga hatujapata taarifa zozote
kutoka kwa wapinzani wetu kuhusiana na tarehe ya kutua nchini, labda
kitu kikubwa nitakachokisema ni kuwa sisi tumejiandaa kupata ushindi
kwenye mechi hii ya nyumbani.
"Na
kwa kuwatumia wachezaji wetu, Chirwa na Zullu, pia benchi letu la
ufundi chini ya Lwandamina na msaidizi wake Mwandila wote wanaotokea
nchini Zambia tutapata ushindi.
"Uongozi
unaamini kuwa, unawajua kabisa Zanaco na hasa wale wachezaji hatari kwa
ajili ya kudhibiti mbinu zao ili kuanzia mechi ya hapa nyumbani na
ugenini zote tupate ushindi," alisema Mkwasa.
No comments:
Post a Comment