Nahodha
wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi, amesema kuwa Yanga wenyewe walijitakia
suluhu kwa woga wao wa kumchezesha Kelvin Yondani nafasi ya kiungo namba
sita.
Timu
hizo, zilivaana wikiendi iliyopita kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara mchezo
uliopigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na kumalizika kwa suluhu.
Suluhu
hiyo, imeifanya Yanga iendelee kukaa katika nafasi ya pili kwenye
msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 53, huku Simba wakiendelea kuongoza
wakiwa na 55.
Nditi
alisema Yanga ilikufa kwenye safu ya kiungo kutokana na kumchezesha
beki wa kati nafasi ya kiungo na kujikuta muda mwingi wakizuia kuliko
kushambulia.
Nditi
alisema, katika mechi hiyo umakini mbovu wa washambuliaji wao ndio
uliowanyima ushindi kutokana na kutengeneza nafasi nyingi za mabao.
“Wakati
timu zinajipanga uwanjani kwa ajili ya kuanza mechi na kumuona Yondani
akichezeshwa namba sita, nikajua kabisa Yanga hawatoki salama.
"Kwa
sababu Yondani nafasi anayomudu kuichezea vizuri kabisa ni namba tano
au nne, lakini siyo sita, hivyo nikajua Yanga wamekuja kulinda goli lao
na siyo kushambulia.
"Hivyo,
tukatumia udhaifu wa Yanga kwenye safu ya kiungo ambayo ilikufa kwa
ajili ya kupeleka mashambulizi golini kwetu, lakini upungufu wa safu ya
ushambuliaji tukakosa ushindi katika mechi hii," alisema Nditi.
No comments:
Post a Comment