MSHAMBULIAJI wa Simba Laudit Mavugo, amesema goli alilofunga dhidi Yanga
anamzawadia bibi yake ambae yupo Bunjumbura ambae alikuwa anamuombea
kwa muda mrefu kabla ya mechi dhidi ya Yanga.
Mavugo alifunga goli la kusawazisha dhidi ya Yanga na huku likiwa ni
goli lake la kwanza dhidi ya Yanga katika mechi mbili za ligi alizocheza
dhidi yao.
Mavugo amesema: “Goli nililofunga ninampatia bibi yangu kama zawadi kwa
sababu amekuwa akiniombea na kunitia moyo kuelekea katika mchezo huo.”
“Kufunga kwangu ni kutokana na kujituma na kuwasikiliza walimu
wanachotufundisha pindi tunapokuwa mazoezini, hiyo ndiyo siri yangu ya
upachikaji wa mabao kwasasa,” alisema Mavugo.
Mshambuliaji huyo raia wa Burundi amesema ana washukuru mashabiki wa
Simba kwa kuwasapoti kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho na kwaahidi
kuwapa kitu ambacho walikikosa takriba miaka minne.
No comments:
Post a Comment