Hii
leo Jumamosi Simba na Yanga zinashuka uwanjani katika mchezo wa Ligi
Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam lakini suala la
tiketi limezua mambo.
Ni
kwamba, mashabiki wa timu hizo mbili wameonekana kugomea baada ya mauzo
ya tiketi mpaka kufikia jana jioni kusuasua tofauti na ilivyotarajiwa.
Meneja
Miradi wa Kampuni Selcom inayosimamia zoezi la uuzaji wa tiketi za
mechi hiyo, Gallus Runyeta amesema kuwa, mpaka kufikia muda huo walikuwa
wameuza tiketi zisizozidi 30,000 ukilinganisha na idadi ya kadi za
kununulia tiketi hizo walizozitoa kwa mashabiki hao.
“Mambo
siyo mazuri kabisa kwani zoezi la tiketi linasua kabisa na ukizingatia
mechi inachezwa kesho (leo), kwani mpaka sasa tumeshauza tiketi
zisizozidi 30,000 tu.
“Tangu
utaratibu wa kuingia uwanjani kwa mfumo huu wa tiketi za kielektroniki
tumeshatoa kwa mashabiki kadi za kununulia tiketi za kuingilia uwanjani
zaidi ya 200,000,” alisema Runyeta na kuongeza kuwa:
“Tiketi
tunazotakiwa kuuza kwa mashabiki ni 57,310 lakini hadi sasa tumeuza
idadi hiyo ya tiketi, sijui tatizo ni nini. Tumeshawasiliana na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwataarifu juu ya hilo,” alisema
Runyeta.
No comments:
Post a Comment