Thursday, February 22, 2018

TANZIA; CANNAVARO APATA MSIBA AKIWA SHELISHELI

WAKATI akipambana kuitumikia klabu yake iliyoko nchini Shelisheli kucheza mechi za kimataifa, nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amepatwa na msiba baada ya kufiwa na mwanaye Anuary Nadir aliyekuwa na umri wa miezi miwili usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Cannavaro anatarajia kuwasili nchini leo akitokea Shelisheli ambako amekwenda kuitumikia Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya St Louis. Yanga ilipata sare ya mabao 1-1 na kusonga mbele huku Cannavaro akicheza kwa dakika 90.

No comments:

Post a Comment