Kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema Yanga haina jeuri ya kuifunga timu yake hiyo ya zamani katika mchezo wao wa leo Jumamosi kwani Wekundu wa Msimbazi wana kikosi imara.
Julio
amesema huko nyuma Yanga iliinyanyasa Simba kwa kuwa haikuwa na kikosi
imara kama ilivyo sasa, hivyo leo ushindi kwao ni jambo la kawaida.
Simba
inaongoza ligi ikiwa na pointi 51 katika mechi 22 ikifuatiwa na Yanga
yenye pointi 49 katika michezo 21. Timu hizo zinakutana leo Jumamosi
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza
na Julio alisema kuwa, Simba ni lazima ishinde ili kudhihirisha uwezo
wa timu yao na dhamira ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.
“Simba
lazima wawe mabingwa msimu huu kuhakikisha tunashinda Jumamosi (leo),
timu inacheza vizuri na wachezaji wanacheza kitimu hivyo Yanga wasahau
suala la kutwaa ubingwa msimu huu. “Kuhusu ligi ya safari hii haina
ushindani mkubwa kwani timu hazina fedha za kutosha kwani zile za
wadhamini hazijitoshelezi hivyo kusababisha timu nyingine kushindwa
kufanya vizuri,” alisema Julio.
“Ni
Simba na Yanga labda na Azam ndizo zinazoonyesha upinzani wa haki
lakini hizo nyingine zilizobaki ni kama zinajikongoja tu kwani hazina
uwezo wa kupambana na vigogo hao."
No comments:
Post a Comment