Monday, April 23, 2018

MSUVA AZIDI KUNG'ARA MOROCCO

Winga Mtanzania anaicheza Difaa Hassan El - Jadida ya Morocco, Simon Msuva, jana amezidi kung'ara baada ya kufunga bao moja timu yake ilipocheza dhidi ya Raja Casablanca ikiwa Uwanja wake wa nyumbani.

Jadida ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-1 na katika mchezo ambao ulikuwa wa ligi kuu, na kufikisha jumla ya alama 41 na ikirejea kwenye nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi.

Bao jingine la Jadida lilitiwa kimiani na Hamid Ahadad na kuifanya timu hiyo itimize jumla ya michezo 26 msimu huu.

Msuva alijiunga na Jadida akitokea Yanga ya Tanzania, na huu ni msimu wake wa kwanza akiwa na Waarabu hao.

No comments:

Post a Comment