Monday, April 23, 2018

MATOLA AWAPA MBINU HII SIMBA


Baada ya kushangazwa na kiwango kilichooneshwa na Simba katika mchezo wa ligi dhidi ya Lipuli FC, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Seleman Matola, ameitaka timu hiyo kuamka zaidi.

Matola ambaye aliwahi kuwa mchezaji na Kocha Msaidizi wa Simba alishangazwa na Simba kucheza chini ya kiwango walipocheza nayo Jumamosi kwenye mchezo wa ligi.

Kocha alieleza kuwa Simba haikuwa kama ile iyocheza michezo mingine, jambo ambali lilipelekea Lipuli wakaizidi Simba katika umiliki wa mpira.

Kocha ameitaka Simba ili iweze kupata matokeo mazuri dhidi ya Yanga ni vema ikajipanga vizuri na kurekebisha mapungufu kadhaa ambayo yanaikabili timu haswa katika umaliziaji.

Matola aligundua mapungufu hayo walipocheza nayo, hivyo amefikia hatua ya kulishauri benchi la ufundi la Simba kuwa ni vema wakaamka mapema kabla ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi.

No comments:

Post a Comment