Mbunge
Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe amemtembelea Tundu Lissu
nchini Ubelgiji anakoendelea na matibabu ya viungo na saikolojia tangu
Januari 7, 2018.
Lissu
ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki anapata matibabu hayo baada ya
kushambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 akiwa nje ya makazi yake mjini
Dodoma.
Awali
mbunge huyo alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Dodoma siku hiyohiyo
kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Nairobi alikotobiwa hadi Januari 6,
2018 alipohamishiwa Ubelgiji.
Katika
picha mbalimbali zilizotoka jana Februari 11, 2018 ziliwaonyesha
wawili hao wakiwa kwenye mwonekano tofauti wa mazungumzo.
Leo
Februari 12, 2018, Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili
Tanzania (TLS) amesema, “Zitto amekuja kunijulia hali na kwa ajili ya
kubadilishana mawazo kuhusu hali ya nchi yetu kisiasa, kiuchumi na
kijamii.”
Hata
hivyo, Zitto ambaye ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo amesema hawezi
kuzungumza zaidi kuhusu kile walichoteta na Lissu huku akiahidi baadaye
kutoa taarifa.
No comments:
Post a Comment