jasiriamali, Mtunzi wa vitabu mashuhuri nchini Tanzania na mmiliki wa
kampuniya Global Publishers, Erick James Shigongo amefunguka na
kujiteua mwenyewekuwa balozi wa hospitali ya Muhimbili.
Shigongo amefikia maamuzi hayo baada ya kujionea mabadiliko makubwa
katika utoaji huduma katika hospitali hiyo na kusema kuwa awali alikuwa
anaichukia hospitali hiyo kutokana na mambo mbalimbali ya hovyo ambayo
yalikuwa yakitokea kipindi cha nyuma kitu ambacho kwa sasa hakipo tena.
"Mimi Eric Shigongo James, Leo Februari 12, 2018, nimeamua kujiteua kuwa
Balozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, iliyopo Muhimbili jijini
Dar es Salaam. Uamuzi huu nimeufikia kwa hiari yangu, bila kushinikizwa
wala kuteuliwa na mtu yeyote, kwa sababu sina chembe ya shaka kwamba
huduma zinazotolewa na taasisi hii ni bora, za kimataifa na zinaliletea
sifa kubwa taifa letu. Nakiri kwa kinywa changu, Mungu shahidi yangu,
kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na vitengo vyake vyote,
imebadilika! Kwa hili nimshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk John Pombe Magufuli kwa kufanikiwa kupandikiza uzalendo,
uadilifu na nidhamu ya kazi ndani ya mioyo ya Watanzania"
Aidha Shigongo amemuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuendelea
kuisaidia hospitali hiyo ya Muhimbili kwa ruzuku na vitendea kazi ili
izidi kutoa huduma bora zaidi na kuokoa maisha ya Watanzania.
"Nimuombe, kwa mikono yote miwili, aiwezeshe hospitali hii kwa ruzuku,
vifaa vya kutendea kazi na motisha kwa wafanyakazi ili iendelee kuokoa
maisha ya Watanzania ambao wengi walikuwa wakifa kwa magonjwa ambayo
yaliweza kutibika tu katika mataifa ya nje na si hapa nyumbani, jambo
ambalo kwa hivi sasa halipo tena; kwani magonjwa makubwa ya moyo
yanatibiwa hapahapa nyumbani na madaktari wetu wa Kitanzania"
Mbali na hilo Shigongo aliweka wazi jambo kuu lililomfanya yeye mwenyewe kujiteua kuwa Balozi wa Muhimbili
"Niliyoyashuhudia ndugu zangu ndiyo yamenifanya niamue kujiteua mimi
mwenyewe kuwa Balozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na
Hospitali ya Muhimbili, ndugu zangu Muhimbili imebadilika, si ile ya
zamani, madaktari wanafanya kazi zao vizuri, wauguzi wanahudumia kwa
kauli nzuri, dawa zipo ilimradi uwe na kadi yako ya bima, hakuna mbu
Muhimbili kama ilivyokuwa zamani"
No comments:
Post a Comment