Friday, February 24, 2017

WACHINA WAMPIGA CHANGA LA MACHO WASTARA

STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma (pichani) amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutapeliwa mamilioni ya fedha na kampuni moja ya simu ya Wachina baada ya kuingia nao mkataba wa kuwa balozi wao hapa nchini.

Wastara aliingia mkataba na Wachina hao mwaka jana ambapo alitakiwa awe analipwa shilingi milioni 400 kwa mwaka lakini ghafla Wachina hao wakaingia mitini.

Akizungumza na Ijumaa kuhusu kutapeliwa huko, Wastara alisema:

“Pesa ambayo nawadai ni kama milioni 84. Kabla ya wao kuja nchini walitaka nianze kutumia pesa zangu kuandaa tisheti, kofia na mambo mengine ya kipromosheni. Kila nikiuliza kwamba mbona simu zenyewe haziji, maelezo yakawa kwamba wameagiza mzigo nje ya nchi, walipoona nawasumbua wakaingia mitini.

“Ilipopita miezi mitatu bila kuona maendeleo yoyote nilianza kuwasiliana nao tena, wakaanza kuniletea Kiswahili kingi, nikashtuka na kuweka mwanasheria wangu amba ambaye alikuwa nao sambamba, napo wakajaribu kumnyamazisha kwa pesa wakashindwa,” alisema Wastara.

Akaongeza kuwa, mara ya mwisho walikwenda kwenye kikao cha kujua hatima ya malipo yake na kinachoendelea ndipo afisa masoko wa kampuni hiyo aliyefahamika kwa jina la Raymond Kalika alipomwambia kuwa Wachina hao wamerudi kwao.

“Yaani nahitaji msaada wa serikali ili nipate pesa zangu,hawawezi kunidhulumu kiasi chote hicho cha pesa katika kipindi kigumu kama hiki,” alisema Wastara. Baada ya kuzungumza na Wastara, Ijumaa lilimwendea hewani Raymond ambaye ndiye aliyemuunganisha Wastara na Wachina hao ili kupata ukweli ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Ukweli wote nimeshamwambia Wastara, hapa tunasubiri hatua zifuatwe, siwezi kuwa na maongezi zaidi ya hayo.

No comments:

Post a Comment