Mgombea
Ubunge wa jimbo la Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalimu asesema kwamba
hoja ya Uzanzibar inayokuzwa na wapinzani wake kwenye siasa hasa kipindi
hiki cha uchaguzi si jambo jema na haifai kuingia kwenye mjadala kwani
inaweza kulipasua Taifa.
Akizungumza
kuhuhusu tuhuma za U-zanzibar dhidi yake, amesema kwamba anajua kwamba
wakati wa vita zinatumika silaha mbalimbali lakini ni vema kwenye hili
la la kuleta Utanganyika na U-zanzibar likatumiwa kwa tahadhari ili
lisije kuleta madhara.
Akiweka
wazi utambulisho wake wa Uzaa, ndg Mwalimu amesema kwamba hajawahi
kuuficha utambulisho wake wa kwamba yeye ni ni mzaliwa wa Zanzibar na
wala haoni kama ni jambo la ajabu.
"Sifa
kubwa ya kuwa mgombea wa ubunge ni uwe raia wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na hapo ikimaanisha Tanganyika na Zanzibar. Sasa kama
chokochoko hizo zimeanza basi watuambie kwamba Zanzibar nchi yenu hii
hapa na Tanganyika tuione ili wazanzibar wawe wanagombea Zanzibar na
Watanganyika wagombee bara. Mimi ni Mzanzibar na wala hilo siyo jambo la
ajabu" Mwalimu
Hata
hivyo Ndg. Mwalimu ameshangazwa na hoja hii kunyooshewa vidole kwake na
kuhoji au huenda yeye siyo mtoto wa Kigogo wa Serikali au CCM ndiyo
maana imeelekezwa kwake na kusema mbona wapo viongozi kibao kama Waziri
Mwinyi na wengineo waliwahi kuwa viongozi bara huku wakiwa na asili ya
Zanzibar na wengine wenye asili ya Tanganyika wakiwa viongozi huko
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment