Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amesema Serikali inajitahidi kujenga na kutanua vituo vya Afya ikiwa na
lengo la kupunguza msongamano kwenye hospitali za Wilaya.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo jana wakati wa kuweka jiwe la msingi la
upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole kilichopo mjini Mafinga.
Makamu
wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo
mkoani Iringa ambapo jana alitembele wilaya ya Mufindi na kuweka mawe
ya msingi katika miradi miwili ikiwa mmoja ni wa kujenga maabara ya
kisasa na madarasa na kidato cha tano na cha sita katika Sekondari ya
Mgololo na upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.
Akiwahutubia
wananchi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la Upanuzi
wa kituo cha Afya Ihongole , Makamu wa Rais alisema katika kila kituo
cha afya kinachopanuliwa ama kujengwa Serikali imezingatia huduma za
mama na mtoto ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto, kuborsha
huduma za upasuaji .
Serikali
imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho na
kutumia mafundi wa kawaida kujenga ilikuweza kusaidia kutoa ajira kwa
vijana zaidi wa eneo husika.
Makamu
wa Rais amezitaka halmashauri zisimamie utoaji na matumizi ya fedha
wanazotoa kwa Vijana asilimia 5 na Wanawake asilimia 5 ili kuleta tija
kwenye shughuli za maendeleo.
Makamu
wa Rais alisema “tunapozungumzia uchumi wa viwanda lazima tuwaandae
Vijana tangia wadogo, tuhakikishe wanafundishwa yale yanayohitajika”.
Makamu
wa Rais aliwaambia wakazi wa Mafinga, watakapokuja tena kwenye kampeni
watawataka wananchi waseme Serikali yao imewafanyia nini.
Mapema
jana Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na
madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Mgololo,
ujenzi ambao utagharimu shilingi milioni 450 za kitanzania chini ya
ufadhili wa kiwanda cha Mufindi Paper Mills.
No comments:
Post a Comment