Monday, May 22, 2017

WATU 141 WAKAMATWA INDONESIA,NI BAADA YA KUSHIRIKI SHEREHE YA WAPENZI WA JINSIA MOJA

Mapenzi kati ya watu wa jinsia moja sio marufuku kulingana na sheria za Indonesia, isipokuwa katika mkoa wa kihafidhina wa Aceh.

Polisi nchini Indonesia wamewakamata wanaume 141 ambao walikuwa wanahudhuria sherehe ya wapenzi wa jinsia moja katika mji mkuu wa Jakarta, siku ya Jumapili.

Polisi wanasema kila aliyehudhuria, akiwemo raia mmoja wa Uingereza na mwingine wa Singapore walilipa kiingilio cha rupiah elfu 185 (dola 14; pauni 10).

Indonesia imeshuhudia kuongezeka kw
a chuki kwa watu wa jinsia moja.

Mapenzi kati ya watu wa jinsia moja sio marufuku kulingana na sheria za Indonesia, isipokuwa katika mkoa wa kihafidhina wa Aceh.

Lakini msemaji wa polisi wa Jakarta Raden Argo Yuwono alisema baadhi ya wale walio kizuizini wanaweza kushtakiwa chini ya sheria kali ya Indonesia ya kupambana na vitendo vichafu.

Mapema mwezi huu polisi huko Indonesia waliwakamata watu wengine katika mji wa Surabaya.

"Baadhi yao walipatikana wakiwa wamevua nguo na wakijitosheleza wao wenyewe kingono, katika eneo la tukio," aliiambia BBC Indonesia.

Chini ya sheria hizo kali za Indonesia, kuandaa onyesho kama hili ili kuwatumbuiza watu inaweza kufasiriwa kama kitendo kichafu.

Wiki iliyopita, wanaume wawili walihukumiwa kifungo cha kuchapwa viboko mbele ya umma katika mkoa wa Aceh, baada ya kupatikana wakifanya ngono. Sheria kali dhidi ya uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja zilianzishwa huko mwaka wa 2014.

Mapema mwezi huu, polisi huko Indonesia w
aliwatia mbaroni watu 14 katika mji wa Surabaya.

No comments:

Post a Comment