Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salumu mwishoni mwa
wiki iliyopita alizua utata katika kona mbalimbali za kijamii kufuatia
kufanya dua maalumu ya kumwombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Freemason Afrika Mashariki, marehemu Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy
Chande’ (pichani).
Tukio hilo lilifanyika Aprili 21, mwaka huu katika Shule ya Sekondari ya
Shabani Robert na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi, akiwemo
Rais Msaatafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa sanjari na
wanafunzi wengine waliowahi kusoma katika shule hiyo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Freemason Afrika Mashariki, marehemu Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy Chande’. |
HABARI KAMILI
Sir Andy Chande alifariki dunia, Aprili 7, mwaka huu nchini Kenya kwa
maradhi ya presha na kuzikwa katika Makaburi ya Baniani, Makumbusho
jijini hapa kwa kuchomwa moto.
Katika enzi za uhai wake, Sir Andy Chande aliwahi kuweka wazi kuwa yeye
ni mfuasi na kuhani mkuu wa Jumuiya ya Freemason, jumuiya ambayo
inaaminika na baadhi ya watu kwamba iko kinyume na mafundisho ya dini za
Kiislamu na Kikristo. Katika tukio hilo la kuwakumbuka waasisi wa shule
hiyo, Shehe Alhadi aliongoza dua maalumu kwa upande wa dini ya Kiislamu
kwa ajili ya kumwombea marehemu Chande jambo lililoibua mjadala mkubwa.
MSIKIE HUYU
Baadhi ya watu walihoji kuwepo kwa shehe mkuu wa Dar kwenye dua hiyo
wakati marehemu alijulikana kuwa ni Freemason ambayo wengi hawaiamini
kama ina sera za Mungu. Msikie huyu:
“Mimi binafsi sidhani kama ni sahihi kumfanyia dua mtu ambaye aliwahi
kuweka wazi kwamba yeye yupo upande wa kushoto, tena akiwa mwenyekiti na
kuhani mkuu wa jumuiya ambayo inaaminika inakwenda kinyume na maadili
ya Kimungu,” alisema Kimashi John katika ukurasa wake wa Facebook.
Mbali na mtu huyo, mijadala mingi siku hiyo ilikuwa kuhudhuria kwashehe mkuu kwenye shughuli hiyo.
Gazeti la Uwazi, baada ya kuyasikia hayo, liliamua kumtafuta Shehe Alhadi mwenyewe ili kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Shehe Alhadi alikuwa na haya ya kusema:
“Katika dua niliyoiomba siku ile hakuna neno nililosema kwamba Mungu aiweke roho ya marehemu
Chande mahali pema peponi. Unaweza kusikiliza tena rekodi za ile dua,
nilichokifanya ni kumwombea kwa Mwenyezi Mungu amlipe kwa mambo yote
aliyoyafanya duniani maana yeye ndiye hakimu wa mwisho.”
Aidha, katika hatua nyingine Uwazi lilipotaka kujua kama alishawahi
kumpa elimu ya dini ya Kiislamu, marehemu Sir Chande ikiwa ni pamoja na
kumtaka asilimu, Shehe Alhadi hakuwa tayari kulizungumzia hilo zaidi ya
kukiri kwamba amekuwa akifahamiana na marehemu kwa muda
mrefu.
No comments:
Post a Comment