Friday, March 24, 2017

HISTORIA YA PESA ZA SARAFU TANZANIA


Riyal

Kabla ya mwaka 1884, nchi yetu ilikuwa inatumia sarafu moja ya Riyal iliyokuwa imetolewa na Sultan wa Zanzibar chini ya Sultani wa Oman. Sarafu za Riyal zilikuwa kama ifuatavyo




 Baada ya 1884, Zanzibar ilitumia sarafu za aina tatu kwa mpigo. Sarafu ya kwanza ilijulikana kama Maria Theresa Thaler iliyotolewa Italy, ilikuwa na sura ifuatayo.

Maria Theresa Saler

 Sarafu ya pili ilikuwa ni rupia ya kihindi pamoja na visehemu vyake ambavyo vilikuwa vingi kidogo. Sehemu kubwa za rupia zilikuwa ni Anna, pice , robo rupia na nusu rupia:

1 Anna

1 rupee 

 1/4 rupee

1/2 rupee

Pesa hizi zilikuwa ngumu sana hasa kwa vile Anna ilikuwa na vipande vingine kama 1/12 ya Anna, 1/6 ya Anna, 1/4 ya Anna na kadhalika. Sikuweka picha za vipande hivi ingawa ninavyo.

Sarafu ya tatu ilikuwa inajulikana kama Zanzibari Rupee ambao kimsingi ilikuwa sawa na rupee ya kiingereza iliyokuwa ikutumika Kenya na Uganda. Sikupata picha yake.

Kwa upande wa bara, kuanzia mwaka 1884 ilikuwa inatumia Rupie za kijerumani. Rupie moja ilikuwa imegawanyika katika pesa 64. Neno la kiswahili "pesa" linatokana na sehemu hii ya rupie.

Pesa 1

Rupie 1


Mwaka 1891 ziliongezwa sarafu za robo rupie na za nusu rupie kama ifuatavyo.

1/4 rupie

1/2 rupie

Ilipofika mwaka 1893 ikaongezwa sarafu ya rupie 2 iliyoonekana kama ifuatavyo

 2 Rupee

Sarafu zote hizo ziliendelea kutumika hadi mwaka 1904 ambapo sarafu ya rupie iligawanywa katika vipande mia moja (decimalization), kila kipande kikijulikana kama "heller." Neno la kiswahili "hela" limetokana na mgawanyo huo. Sarafu za
nusu heller na heller moja zilitolewa wakati huo zikiwa na sura zifuatazo.

1/2 heller


1 heller

Kipindi hicho, sarafu za robo rupie, nusu rupie, na rupie 1 zilitolewa upya zikiwa na sura zifuatazo:

 1/4 rupie

 1/2 rupie

1 rupie

Mwaka 1908, serikali iliamua kuongeza idadi ya sarafu kwa kuingiza sarafu ya heller 5 na heller kumi zilizokuwa na sura zifuatazo. 

10 heller

 5 heller 


Sarafu hizi ziliendelea kutumika hadi vita ya kwanza ya dunia ilipoanza mwaka 1916. Mwaka huo serikali ilitoa sarafu ambazo hazikuwa zimetengenezwa kwa ufundi kabisa. Sarafu zilizotolewa wakati huo zilikuwa zile za heller 5, heller 20 na rupie 15. Sarafu za heller 5 na heller 20 zilikuwa na sura ifuatayo.

heller 5

 heller 20

 Sarafu ya rupie 15 ilikuwa ya dhahabu, ilijulikana kama "Tabora Pound." Ni kati ya sarafu ambazo zilikuwa ghali sana katika historia ya nchi. Kwa bahati mbaya siyo sarafu nyingi zilizoingia kwenye mzunguko kutokana na vita, kwa hiyo nyingi ziliishia kwenye minada ya wakusanya sarafu. Sura yake ilikuwa kama ifuatavyo

No comments:

Post a Comment