Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amekaribisha waliokuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwamo aliye
Alisema
wanachama hao walikuwa mashujaa wa kutetea haki, demokrasia na
taratibu kwa kupinga dhuluma ndani ya chama chao cha CCM.
“Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.
“Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwatajwa huko katika vikao vyao.
“Wamewatimua
wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao
kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.
“Nataka
kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na
demokrasia na misingi ya utawala bora nchini,” alisema Lowassa katika
taarifa yake
Mjumbe
huyo wa Kamati Kuu alisema wanachama hao wa CCM walisimamia kile
walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na
uonevu.
“Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.
“Baba
wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba upinzani wa kweli
utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa.
“Nawakaribisha
Chadema na Ukawa kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna
minyororo ya utumwa wa siasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura
teke unamuongezea kasi tu.
“…waje
wajiunge nasi katika safari ya kuleta demokrasia ya kweli na siasa
zenye ukomavu, safari hii inahitaji umoja na mshikamano kufikia
malengo,” alisema.
Lowassa alisema anashangazwa na namna hatua ya CCM kujinasibu kuwa CCM ikiyumba.
Alisema
nchi itayumba lakini anaamini kinachotokea na jinsi CCM inavyoyumba
ndivyo wananchi wanavyozidi kukomaa katika siasa na kuimarika katika
harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.
Alisema Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala.
“Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora,” alisema.
Juzi,
CCM kilitangaza kuwafukuza wanachama wake 12, akiwamo Mwenyekiti wa
Umoja wa Wanawake (UWT), Sophia Simba, ambaye wiki iliyopita alitangaza
kutogombea tena nafasi hiyo.
Wengine
waliofukuzwa ni wenyeviti mikoa ambao ni Jesca Msambatavangu (Iringa),
Erasto Kwilasa (Shinyanga), Ramadhan Madabiba (Dar es Salaam) na
Christopher Sanya (Mara).
Waliofukuzwa
wengine ni Willfred ole Mollel ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Arusha Mjini, mjumbe wa NEC wa Wilaya ya Babati Mjini, Ally Sumaye na
Mathias Manga wa Wilaya ya Arumeru.
Katika
orodha hiyo pia wamo wenyeviti wa wilaya wa chama hicho ambao ni Omari
Awadhi (Gairo), Ally Msuya (Babati Mjini), Makolo Laizer (Longido) na
Salumu Madenge (Kinondoni-Dar es Salaam).
Wanachama
wengine waliochukuliwa hatua baada ya kufanya makosa kama hayo kuwa ni
Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ambaye amepewa onyo kali na anatakiwa kuomba
radhi.
Wakati
Nchimbi akipewa onyo, Adam Kimbisa ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Dodoma na Mbunge wa Afrika Mashariki amesamehewa.
Kutokana
na uamuzi huo Sophia atalazimika kupoteza ubunge. Ilielezwa kuwa
amefukuzwa baada ya kupatikana na makosa ya maadili kinyume na Katiba na
kanuni za chama hicho.
No comments:
Post a Comment