Rais
wa Marekani Donald Trump amelielezea shambulio la kuhusisha gesi yenye
kemikali zenye sumu dhidi ya watu wakati wa mashambulizi ya anga
kaskazini mwa Syria kuwa ni tukio lisilo la kibinaadamu.
Marekani na mataifa mengine ya magharibi yamemshutumu Rais wa Syria,
Bashar Assad na serikali yake kwa kile walichodai shambulio la kutumia
silaha za kemikali la siku ya jumanne mjini Khan Sheikhoun.
Trump amesema vifo vya watoto vimebadili mtazamo wake kwa Assad.
'na nitakueleza, kuwa shambulio lile dhidi ya watoto limenifanya niwe na
mtazamo mwingine.
Ni kitu cha kutisha inatisha sana, na nimekuwa
nikifuatilia na kutazama, hakuna namna nyingine zaidi naweza kusema,
imekwishatokea kuwa sasa mtazamo wangu kwa Syria na Assad umebadilika
sana.''
Marekani, Uingereza na Ufaransa, zote zimemshutumu mshirika wa Serikali
ya Syria kwa kile kilichotoka katika mji wa Khan Sheikhoun.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson ambaye anatarajiwa
kufanya ziara mjini Moscow nchini Urusi juma lijalo, ameitaka Urusi
ifikiri kwa makini kuhusu uhusiano wake na Syria.
Hakuna shaka yeyote kuwa utawala wa Syria chini ya Bashar Al Assad
unahusika na shambulio hili la kinyama na tunaona sasa ni wasaa kwa
warusi kufikiri kwa makinni kwelikweli kuhusu kuendelea kuunga mkono
utawala wa Assad''
Urusi imepinga msimamo wa marekani na mataifa ya magharibi kuhusu tukio
hilo na kusema kuwa , mswada kuhusu azimio la baraza la usalama la umoja
wa mataifa kuhusu shambulio hilo ni chuki dhidi ya Syria
No comments:
Post a Comment