Wednesday, April 5, 2017

UHARIBIFU WA MAZINGIRA KATIKA MTO NAWI


CHANZO cha uharibifu wa mazingira katika mto Nawi uliopo katika kijiji cha Nguni Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro imeelezwa kuchangiaku kosekana  kwa maji katika maeneo ya ukanda wa tambarare katikawilaya hiyo.

Uharibifu huo ambao umefanywa na baadhi ya wananchi kwa kufanya shughuli za kinadamu bila kujali  madhara ya shughuli  wanazozifanya kumepelekea wananchi kukosa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pamoja na kukwamisha kilimo cha  umwagiliaji .

Akizungumza katika zoezi la upandaji miti katika mto huo , diwani wa kata ya Masama kati Deogratius Kimaro  alisema shughuli za  kibidamu zinazofanywa katika mto huo unaotegemewa kupelekea maji kwa wananchi wanaoishi ukanda wa tambarare na  kukosa maji hali ambayo imepelekea kupungua kwa maji  na kushindwa kufanya shughuli nyingine za uzalishaji.

“Ndugu wananchi shughuli mnazofanya katika mto huo zimesabisha madhara makubwa kwa wakazi wa ukanda wa tambarare na hata sisi wa ukanda huu kwani maji ni machache kwenye  mto huu kutokana na sisi mwenyewe kulima kwenye vyanzo pamoja na kukata miti ambayo ilisaidia kuboresha uoto wa asili” alisema Kimaro.

Alisema , jukumu la utunzaji wa mazingira ni la kila mmoja na kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa baadhi ya jamii kuona kuwa zoezi la utunzaji  wa mazingira ni la serikali kitu ambacho si sahihi na kuwataka kuondokana na dhana hiyo.

Nae mkazi wa kijiji hicho Onesmo  Kileo alisema kuwa shughuli za kibinadamu zinaendelea katika vyanzo vya maji kutokana na dhana iliyojengeka kwenye jamii kuwa maeneo hayo ni ya urithi na
wanayamiliki kihali na kuamua kufanya shughuli hizo.

Kwa upande wake ofisa misitu wa kata, Masama Mashariki John  Katikirwa, alisema wanakabiliana changamoto kubwa katika zoezi la kudhibiti hali ya uharibifu wa mazingira kutokana na baadhi ya viongozi kushirikiana na watu wanaohusika na uharibifu  mazingira.

Hata hivyo Katikirwa alisema zoezi la upandaji wa miti litakuwa endelevu kwa lengo la kurudisha hali ya uoto wa asili uliopotea kutokana na baadhi ya watu kukata , kulima  na kuchoma miti katika

maeneo yalitengwa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira


No comments:

Post a Comment