Mgororo
wa ruzuku ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) unazidi kupamba moto baada
ya mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kwenda kuitetea mahakamani.
Profesa
Lipumba na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa chama hicho, Thomas Malima
wamefungua maombi Mahakama Kuu wakiomba waunganishwe kwenye kesi
iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa CUF, walio upande wa Katibu Mkuu,
Maalim Seif Sharif Hamad.
Katika
kesi ya msingi ya ruzuku namba 21 ya mwaka 2017, wadai wanaiomba
Mahakama imzuie msajili kutoa ruzuku kwa CUF na imuamuru Sh360 milioni
alizozitoa kwa kina Profesa Lipumba zirejeshwe kwenye akaunti rasmi ya
chama.
Wadaiwa
katika kesi hiyo ni Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, lakini Profesa Lipumba na Malima wamewasilisha maombi
mahakamani nao waunganishwe kwenye kesi hiyo upande wa wadaiwa.
Maombi
hayo yalitajwa jana na Malima aliieleza mahakama wakiwa viongozi halali
wa chama hicho, wanaomba kujumuishwa kwenye shauri hilo kwa kuwa wana
masilahi na shauri hilo.
Wakili
wa CUF upande wa Katibu Mkuu, Juma Nassoro na Wakili wa Serikali, Hang
Chang’a waliieleza mahakama kuwa bado hawajapewa hati za maombi hayo.
Jaji
Wilfred Dyansobela aliamuru waombaji hao (kina Lipumba) kuwapatia
nyaraka hizo na amepanga kusikiliza maombi hayo Juni 6, siku ambayo kesi
ya msingi itatajwa.
No comments:
Post a Comment