Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kesi ya mauaji inayomkabili mke wa
marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41) na mfanyabiashara
Revocatus Muyela (40) ipo kihalali mahakamani hapo.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Thomas Simba alitoa uamuzi huo jana dhidi ya hoja
zilizowasilishwa na upande wa utetezi unaodai kesi hiyo namba 5 ya 2017
imefunguliwa kinyume na sheria ukitaka ifutiliwe mbali.
Hakimu Simba alisema upande wa utetezi unaweza kuwasilisha rufaa Mahakama Kuu kama hawajaridhika na uamuzi huo.
“Nimepitia
maombi yaliyoletwa na upande wa utetezi na majibu yaliyotolewa na
upande wa mashtaka, nimegundua lugha iliyotumika ni kuachia lakini
Jamhuri ina uwezo wa kuwakamata tena na kuwashtaki.” alisema Simba
Wakili
wa Serikali, Patrick Mwita alisema upelelezi wa shauri hilo
haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa. Hakimu
aliiahirisha kesi hiyo hadi Mei 4.
Februari
23, washtakiwa Mrita na Muyela waliachiwa huru na Mahakama mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kisha wakakamatwa na baadaye
kusomewa mashtaka ya mauaji upya.
Kwa
pamoja wanadaiwa kumuua kwa kukusudia Aneth Msuya, ambaye ni dada wa
marehemu bilionea Msuya, Mei 25, 2016, eneo la Kibada, Kigamboni Dar es
Salaam.
Awali,
baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka ya mauaji wakili wao, Peter
Kibatala aliiomba Mahakama kufuta kesi hiyo akidai imefunguliwa kinyume
na sheria kwa kuwa ilishafutwa.
Alidai
kesi hiyo ilifunguliwa kinyume na sheria kwa sababu ilishatolewa uamuzi
Februari 23 na Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa aliyewaachia huru.
“Hakimu
Mwambapa katika uamuzi wake aliwaachia huru na hawakupaswa kukamatwa na
kuletwa tena mahakamani kusomewa shtaka jipya la mauaji.Bali upande wa
mashtaka ulipaswa kuomba marejeo Mahakama Kuu au kukata rufaa,” alidai wakili huyo wa utetezi.
Alidai Mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kulipokea jalada jipya na kuwasomea washtakiwa mashtaka yao kwa kuwa limeshatolewa uamuzi mahakamani hapo.
Alidai Mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kulipokea jalada jipya na kuwasomea washtakiwa mashtaka yao kwa kuwa limeshatolewa uamuzi mahakamani hapo.
Wakili
wa Serikali Kishenyi Mutalemwa alipinga hoja hizo na kudai washtakiwa
wamesomewa shtaka hilo kwa mujibu wa sheria na kwamba, uamuzi uliotolewa
na upande wa mashtaka ulikuwa na nafasi ya kuwakamata kuwasomea shtaka
hilo la mauaji.
No comments:
Post a Comment