Mnamo dakika ya 10 Henrikh Mkhitaryan alikata utepe baada ya kuzifumania nyavu za Anderlecht ingawa Sofiane Hanni alisawazisha dakika ya 32.
Wale wasioipenda Manchester United pengine usiku wa kuamkia leo wamekuwa na furaha mpaka dakika ya 107 ya mchezo pale mchezaji kinda Marcus Rashford alipoutumia muda wa nyongeza kuivuruga Anderlecht na kufanikiwa kuipeleka Man U katika nusu fainali ya Europa League.
Manchester sasa inaelekeza nguvu zake katika Premier League wanaposafiri kwenda kukutana na Burnely Jumapili. Tutakutangazia mechi hii kwa kiswahiuli hiyo jumapili. Kabla ya hiyo ya jumapili, jumamosi tutakuwa tumekutangazia mtanange wa West Ham dhidi ya Everton.
Leo ndiyo siku ambayo droo ya Champions League na ile ya Europa League zinatangazwa. Yaani leo ndiyo inafahamika nani anakutana na nani katika nusu fainali. Manchester United inaweza kukutana Ajax ya Uholanzi, Celta Vigo ya Hispania au Lyon ya Ufaransa. Upande wa Champions League zimesalia Real Madrid, Juventus, Monaco na Atletico Madrid. Droo hizi zitafanyika katika makao makuu ya UEFA mjini Nyon, Switzerland.
No comments:
Post a Comment