Sunday, February 12, 2017

YUSUPH MANJI ALIVYOCHUKULIWA NA GARI LA WAGONJWA POLISI NA KUPELEKWA HOSPITALI

Mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti wa Club ya soka ya Yanga Yusuph Manji amekua akishikiliwa na Polisi kituo cha kati Dar es salaam toka Alhamisi ya February 9 2017 baada ya kwenda kuhojiwa kutokana na kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye orodha ya watu 65 kwenye sakata la dawa za kulevya.



Jana jioni Mfanyabiashara huyo alichukuliwa na gari la kubebea Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP na  alionekana akitembea na kuingia kwenye gari hilo (Land Cruise Nyeupe) yeye mwenyewe bila kubebwa au kusaidiwa huku gari lake aina ya Range Rover likitangulia mbele na watu wengine.



Baada ya gari hilo kumchukua msafara huo ulikwenda moja kwa moja kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Muhimbili Dar es salaam ambako watu mbalimbali wanaosumbuliwa na moyo hupata matibabu.


Gari la wagonjwa lililombeba Yusuf Manji na gari lake binafsi katika viunga vya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

No comments:

Post a Comment