Manji: Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.
Manji: Mimi
nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi
yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua
ninavyoheshimiwa.
Manji: Na chaguzi zilizopita mimi nilichukuahukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo naheshimika.
Manji: Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri.
Manji: Na katiba inasema kila mtu ana haki yake, Ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima.
Manji: Ukinishutumu mimi ni mpumbavu tu wewe.
Manji: Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari.
Manji: Mimi nitaenda Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.
Manji: Kifungu cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kufungu 32 pia. Vinanilinda.
Manji: Nataka nimshitaki Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.
Manji:
Kesho naenda Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki
yangu. Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.
Manji: Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, Alichofanya mkuu wa mkoa ni kosa siwezi kukubali.
Manji: Na Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.
Manji: Kwanini RC Makonda hajamuita Askofu Pengo au Mashehe wamsaidie?
Manji:
Hiwezi kuniita mimi kama mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho
utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.
Manji: Zipo njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania.
Manji: Kama
unataka msaada omba msaasa sio unaagiza msaada, Unaniita na watu 65
nikae kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Saa tano usiku
nitoke? Sina kazi nyingine za kifanya?
Manji:
Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shilling moja.
Unanihusisha mimi jina langu nloachiwa na baba kwenye huu upumbavu
halafu unathubutu kiniita kaka yako?
Manji: Hii itanifanya nishindwe kwenda Comoro na Klabu ya Yanga sababu Wanacomoro watasema nimepeleka madawa. Wananichafua sana.
Manji: Hivi
ni vita na wanahitaji msaada haraka na kama wana shutuma au ushahidi au
huo msaada wanieleze. Kama vita kwanini isiwe leo wasubiri ijumaa. Mimi
naenda kesho.
Manji: Kesho nyie watu wa magazeti na habari msitoe habari kwa upande mmoja.
Manji: Ambao
hawatabalance habari. Cybercrime inasema ukiweka habari ya uongo
unafungwa. "Ambaye ataandika makonda manji dawa za kulevya" kesho
namshitaki.
Manji: Wakina
Amina Chifupa walitaja majina, yalienda wapi? Hii jitihada hakuna mtu
anakataa. Hata unayemchunguza humtaji kwenye vyombo vya habari. Hata
TAKUKURU hawawataji wanaowachunguza. Mimi siwezi kwenda kutaja mshahara
wa mfanyakazi. Nitakiwa namvunjia heshima.
Manji: Mimi nipo tayari kupimwa na kusearchiwa na Makonda naye apimwe kama anatumia na wamsearch pia.
Manji: Mimi
sitaki kuchanganya vitu viwili kwenye mkutano mmoja. Kesho au
keshokutwa ntafanya mkutano kuanzia PSPF, Coco Beach nk. Leo nakaa
kwenye point moja tu ya madawa.
Manji:
Mkuu wa mkoa kunasehemu nimegongana naye oysterbay na nlienda kuonanana
naye kama diwani wa mbagala kuu kumuomba mkuu wa majeshi atakayekuja
ahamishe kambi ya jeshi kutoka mbagala na kupelekwa nje ya mji. Kama
diwani siwezi kumuandikia rais.
No comments:
Post a Comment