Wednesday, July 12, 2017

WATUMIAJI WA TWITTER WAMPELEKA TRUMP MAHAKAMANI


Rais wa Marekani, Donald Trump ameshtakiwa  na  watumiaji wa mtandao wa Twitter aliowafungia  wasione anachoandika katika ukurasa wake.

Watu saba wamefungua mashtaka katika mahakama moja jijini New York nchini humo wakimtaka rais huyo awafungulie kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha Katiba.

Wanasema kwa kuwa Rais wao huwa anatumia ukurasa wake @realDonaldTrump kutoa taarifa mbalimbali za Serikali, ni haki yao kuona na kujibu anachoandika.

“Ukurasa wake unawawezesha wananchi kuwasiliana naye moja kwa moja hivyo ni haki ya kila raia kuweza kuuona, kutufungia ni sawa na kutunyima haki yetu ya kikatiba ya kupata taarifa,” inasema sehemu ya mashtaka hayo.

Kabla ya kufungua mashtaka hayo, watu hao waliandika barua kwenda kwa Rais Trump iliyokuwa na orodha ya majina yao wakitaka awafungulie waweze kusoma na kujibu anachoandika, hata hivyo, barua hiyo haikujibiwa

No comments:

Post a Comment