Timu ya Simba imewakalisha wapinzani wao wa jadi Yanga kwa mapato jumla ya fedha walizoweza kuingiza katika mechi zao za kimataifa zilizochezwa katika siku mbili tofauti ndani ya dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kusema mechi ya Simba dhidi ya Al Masry ya Misri uliochezwa Jumatano Machi 7,2018 umeweza kuingiza takribani milioni 85 katika fedha zote huku mashabiki elfu kumi na nne mia saba tisini na nane (14,798) wakiwa wamehudhuria kuangalia mtanange huo uwanja wa Taifa.
Kwa upande wa mchezo wa Yanga umeweza kuingiza mashabiki elfu tisa mia tisa sitini na moja(9,961) na kufanikiwa kukusanya zaidi ya fedha milioni 56 za kitanzania katika mchezo wake dhidi ya Township Rollers ya Botswana uliochezwa Jumanne Machi 6,2018.
Kwa upande mwingine, TFF imesema baada ya kumalizika kufanyika kwa mgawanyo wa pesa hizo zote kwa kila mechi timu ya Simba ikapata takribani milioni 43 za kitanzania huku Yanga wakiramba takribani milioni 28 za pesa zote zilizoweza kukusanywa

No comments:
Post a Comment