Mwenyekiti
wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema ameibuka na kusema
kuwa wapo baadhi ya polisi wanagawa na kusambaza dawa za kulevya pia
wanawasaidia baadhi ya waathirika wa dawa hizo waliopo magerezani
kuzipata.
Augustino
Mrema anasema vita ya dawa za kulevya inawezekana kumalizika kama
watawatumia watumiaji na wauzaji wadogo wadogo kuwapata wale wauzaji
wakubwa ambao ndiyo tatizo zaidi katika jamii.
"Vita
hivi vitawezekana kumalizika kama tutatumia hawa wadogo wenye kete
mbilimbili, na siyo kuwapeleka magerezani, wamenionesha na njia
wanazotumia kuwapa dawa waathirika waliopo magerezani, tusitumie nguvu
nyingi kuwakamata hawa dagaa wadogo wadogo, bali tuwatumie hawa tupate
chain nzima, kwa njia hiyo tutapeleka watu wanaostahili magerezani" alisema Augustino Mrema
Mbali
na hilo Augustino Lywatonga Mrema anasema kama polisi walikuwa
wanasambaza na kugawa madawa ya kulevya hivyo basi wao ndiyo walikuwa
wakiendesha hivyo vijiwe na kuwajua wahusika wa madawa ya kulevya.
"Sasa
kama polisi ndiyo anasambaza na kugawa madawa kwa hiyo vijiwe vile
vilikuwa vinaendeshwa na wao, hivyo wanawajua wanaogawa, na wanaotumia
sasa huu mtandao ukikamatwa hii nchi itapona" alimalizia Mrema.
No comments:
Post a Comment