Wednesday, February 8, 2017

JULIO SASA YUKO TAYARI KUCHUKUA NAFASI YA KAHEMELE PALE MSIMBAZI






Add caption


Kocha wa zamani wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema yupo tayari kurejea kujihusisha na soka kwa mara nyingine baada ya kustaafu kwa muda kwa kuomba akabidhiwe majukumu ya ukatibu mkuu wa Simba.


Awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na  Patrick Kahemele ambaye aliamua kujiuzulu na kurejea Azam TV wiki iliyopita.

Julio aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Simba kwa nyakati tofauti alijiweka pembeni kujihusisha na masuala ya soka na kuikacha timu yake ya Mwadui baada ya kuchoshwa na maamuzi mabovu ya waamuzi wa ligi kuu.

Julio amesema kuwa kwa upande wake hana wasiwasi endapo viongozi wa Simba wakiongozwa na rais wake, Evans Aveva wakiamua kumpa nafasi hiyo kwani anaamini ana uwezo wa kuongoza.


“Siyo kama najipigia chapuo lakini kama viongozi wa Simba wakiamua kunipa nafasi ya ukatibu sitaweza kukataa kwa sababu naipenda timu hiyo na kila mmoja anajua na kama nikiwepo naamini nitaongezea kitu fulani na kuifanya timu ipate matokeo mazuri.



“Uzuri wangu kwangu kwamba sikufungiwa na mtu yeyote kujihusisha na soka hivyo hata nikirejea hakuna ambaye atashtuka na niwaahidi kwamba nitaitumikia nafasi hiyo kuleta mabadiliko yaliyoshindikana kwa kipindi kirefu,” alisema Julio.

No comments:

Post a Comment