Taarifa ikufukie kwamba, kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema Simba wamefanikiwa kuweka rekodi hiyo ambayo ni kubwa kwa klabu za hapa Tanzania.
Aidha, Manara ameeleza kama mipango kwa mwaka huu itakuwa imeenda vizuri, kuna uwezekano wa kutoka kiasi hicho cha milioni 200 mpaka 300 endapo hakutakuwa na ulanguzi wa jezi ambazo wametambulisha jana.
Manara amesema endapo wapenzi na mashabiki wa Simba watanunua jezi ambazo ni asili na si bandia, wataisaidia klabu kufikia lengo la kukusanya kiasi hicho cha fedha ndani ya msimu ujao.
Simba imetambulisha jezi zake rasmi jana ambazo zitatumika kwa msimu ujao ambapo nyekundu zitakuwa za nyumbani na nyeupe kwa mechi za ugenini.
No comments:
Post a Comment