KOCHA Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ameanza kutoa mafunzo ya mfumo anaotaka kuutumia katika msimu wa 2018/19 akiwa na Simba.
Simba imeweka kambi katika mji mdogo wa Kartepe ambao uko mlimani kabisa, sehemu maalum kwa ajili ya kambi za timu.
Aussems ameanza kukinoa kikosi chache akiwafundisha mifumo na namna ya uchezaji katika masuala mbalimbali.
Kocha huyo amekuwa akiwaonyesha wachezaji wake namna ya kulinda lakini pia kushambulia kwa tahadhari.
Wakati Simba ilipotua hapa, kocha huyo alianza kutoa mafunzo ya kawaida, zaidi wachezaji wakionekana kupasha misuli kawaida.
Inaonekana amekuwa akiongeza mazoezi taratibu huku akichanganya na aina ya uchezaji.
Makocha wengi huanza kufundisha mifumo baada ya timu zao kupata mazoezi ya kutosha. Lakini Mbelgiji huyo anaonekana kuwa tofauti kidogo akienda anachanganya mazoezi ya kawaida na mifumo, taratibu.
No comments:
Post a Comment