Thursday, May 17, 2018

RC ZAMBIA AWAPA SIKU 3 MAOFISA BIASHARA NA AFYA

Na.Ahmad Mmow.
MKUU wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewapa siku tatu maofisa biashara na afya mkoani humu kumpa taarifa za kina juu ya ukaguzi watakaofanya kwenye maduka yanayouza vyakula,baada ya kubaini baadhi ya wafanyabiashara wanakiuka taratibu na sheria.

Zambi alitoa agizo hilo jana alipotembelea baadhi ya maduka yanayouza vyakula katika manispaa ya Lindi,kuelekea kuanza funga ya saumu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ulioandama jana.

Mkuu huyo wa mkoa wa Lindi alitoa agizo hilo baada ya kubaini baadhi ya wafanyabiashara wanafanyabiashara bila leseni na kukwepa kulipa kodi.Huku wengine wakibainika kuingiza na kuuza bidhaa ambazo hazina risti za manunuzi.

Akitoa agizo hilo alisema ingawa alipewa taarifa na maofisa biashara kwamba bei ya vyakula haijapanda,lakini alilazimika kutembelea maduka ili kujionea na kujiridhisha naukweli wa taarifa hizo.

"Maofisabiashara na afya naomba mfuatilie taarifa za wafanyabiashara hawa.Nafuu ya kodi wamepewa wachuuzi.Sio wenye maduka,nyie mpo,hiyo sio sawa.Hawalipi kodi na hawana leseni.Wengine hawana risti za manunuzi za bidhaa wanazouza" upo uwezekano mkubwa kwamba baadhi ya bidhaa hazikununuliwa na kuingia kihalali na nyingine hazina nembo za ubora na viwango" alisema Zambi.

Katika kuhakikisha agizo lake linafanyiwa kazi kwa usahihi na haraka amewataka maofisa hao kuwasiliana na maofisa wa mamlaka ya mapato(TRA),shirika la viwango(TBS) na mamlaka ya udhibitiubora na usalama wa chakula na dawa(TFDA) ili washirikiane nao wakati wa zoezi hilo la ukaguzi.Ambapo matokeo ya ukaguzi huo akabidhiwe ndani ya siku tatu tangu atoe agizo hilo.

Mbali na agizo hilo kwa watumishi hao wa umma,mkuu huyo wa mkoa amewaonya wafanyabiashara ambao wanatamani kupandisha bei ya vyakula katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani wasipandishe.Kwasababu watachukuliwa hatua kali za kisheria iwapo watapandisha bei hizo ambazo zitawaumiza walaji.Huku pia akiwataka kuzingatia suala la usafi kwenye maeneo yao ya biashara.

"Suala la usafi nilalzima pia,dumisheni nafanyeni usafi katika maeneo ya biashara.Nahilo halitaki siku ya jumamosi.Bali kila siku,mofisa afya fuatilieni pia hilo.Kuhakikisha maeneo yabiashara yanakuwa safi wakati wote," Zambi alisisitiza na kutoa agizo jingine.

Alibainisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya kupandisha bei  za bidhaa,hasa vyakula katika kipindi cha mwezi wa Ramadhani na kusababisha mateso kwa wanaofunga saumu na wasio funga.Hivyo mwezi huo hugeuka nakuwa kama adhabu kwa walaji.

Kuhusu bei ya vyakula alisema vyakula vingi havijapanda bei.Isipokuwa kuwa mafuta ya uto(mafuta ya kula) ambayo hayapo kwa wingi.Bali yanapatikana katika maduka machache.Hata hivyo ongezeko la bei ya bidhaa hiyo sio kubwa kiasi cha kuwaumiza walaji.

Hadi jana bei za vyakula katika mamispaa zilikuwa za kawaida.Huku ikishuhudiwa kushuka kwa bei ya mchele kutoka shilingi 2,800 kwa kila kilo moja juma moja lililopita,nakufikia shilingi 1,700.Huku sukari ikiendelea kuuzwa na kununuliwa kwa shilingi 2,500 kwakila kilomoja.

No comments:

Post a Comment