Nahodha
na beki kisiki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amezitaja mbinu tatu
ambazo watazitumia katika harakati zao za kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu
Bara msimu huu.
Cannavaro
amezitaja mbinu hizo kuwa ni ushirikiano, kujituma uwanjani na kuwa na
nidhamu ya mchezo kwa kila mmoja wao wanapopambana na timu mbalimbali
bila ya kujali ukubwa au udogo wake.
Beki
huyo amebainisha hayo kabla ya mchezo wao wa jana Jumapili dhidi ya
Mtibwa Sugar ambapo walikuwa wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi
52, nyuma ya vinara Simba wenye pointi 55.
“Tutaendelea
kupambana hadi mwisho kuona itakuwaje, hatuwezi kukata tamaa wala
kujiona wapweke kutokana na kuzidiwa pointi na wapinzani wetu.
“Bado
naamini tuna uwezo mkubwa tu wa kutetea taji letu kwa sababu nafasi ya
kufanya hivyo tunayo, tena ni kubwa tu. Ili tufikie malengo hayo, ni
lazima tuwe na ushirikiano baina yetu, tujitume uwanjani na kuwa na
nidhamu ya mchezo bila ya kuonyesha dharau kwa timu yoyote ile
tutakayokutana nayo,” alisema Cannavaro.
No comments:
Post a Comment