Friday, May 18, 2018

GINA HASPEL MWANAMKE WA KWANZA AIDHINISHWA KUIONGOZA CIA MAREKANI


Seneti ya Marekani imeidhinisha uteuzi wa Gina Haspel kama mkurugenzi na mwanamke wa kwanza wa CIA, huku akipigiwa kura na maseneta hamsini na nne kwa kura ya ndiyo na arobaini na tano wakipiga kura ya hapana.

Haspel, mkongwe katika shirika la ujasusi la Marekani, CIA, alikabiliwa na upinzani mgumu wakati wa kunadiwa kwake na hali ya nasaba yake na CIA na mbinu zake za namna ya kuhoji watuhumiwa zilivyokuwa za kipekee.

Gina awali alikuwa msimamizi wa gereza moja la siri lililoko nje ya Marekani ambako watuhumiwa wa ugaidi walikuwa chini ya bweni la maji, aina ya matesa ya kuzamishwa katika kina cha maji ambapo wengi huona kama mateso makubwa.

Bi Haspel amesema sasa CIA haipaswi kutumia tena mbinu za namna hiyo.

Seneta wa chama cha Republican John McCain ni miongoni mwa watu waliokumbana na mateso ya namna hiyo pindi alipokuwa akiteswa kwa miaka mitano kwenye jela mojawapo nchini Vietnam, mapema alipopata fununu za uteuzi wa Gina Haspel , aliupinga uteuzi huo bila kusita .

Miongoni mwao ni , seneta wa Virginia Mark Warner, anamuelezea Gina kuwa aliwahi kumwambia kwamba Shirika hilo halipaswi kutumia mbinu kama hizo, na kuahidi yeye binafsi kutorudia tena hata kama raisi Donald Trump ataamuru kutekelezwa.

Mark anasema anaamini misimamo ya Haspel kwamba anaweza kusimamia kauli zake hata kama raisi ataamuru; yeye hana hofu ya kusema ukweli kwa mamlaka za juu endapo amri zinaweza kuwa haramu ama uovu ndani yake hasiti kukataa kutekeleza na endapo atakubali amri hizo basi kwake itakuwa ni sawa na kurejea kwenye utesaji.

Na huu ndiyo uliokuwa ni wasifu wa Gina kabla ya upigaji kura.Mnamo mwaka wa 2002, alichaguliwa na shirika hilo kuongoza kitengo kilichoitwa "black site" huko nchini Thailand mahali ambako mbinu za mahojiano ya kikatili zilitekelezwa , na ripoti ya seneti ikaita mbinu hizo kuwa ni mateso.

Mtuhumiwa mmoja alipelekwa katika kitengo hicho cha "black site", Abd al-Rahim al-Nashiri, alitendewa ukatili uliopitukia kwa kutumia njia ambazo zilipigwa marufuku baadaye na Rais Barack Obama.

Al-Nashiri, ambaye alifanyiwa mahojiano mara baada ya Bi Haspel kuchukua nafasi hiyo,na kuamriwa kupewa adhabu ya kutopata usingizi, alidhoofishwa kwa kila hali, aliachwa utupu, kuwekwa mahali penye joto kali, kuwekwa kizuizini kwenye boxi boksi dogo ama hata kupigizwa ukutani mara kwa mara.Miaka mitatu baadaye,

Bi Haspel aliamuru kuharibiwa kwa mikanda ya video ipatayo 92 ambazo ndani yake alionekana akifanya mahojiano hayo na Al-Nashiri, pia Abu Zubaydah, ambay pia alikuwa akishikiliwa mahali fulani nchini Thailand.

Inakadiriwa kuwa wanaume wapatao 119 walipitia mateso makubwa mara baada ya shambulio ya majengo pacha na wizara ya ulinzi ya Marekani, na hii ni kwa muujibu wa ripoti ya seneti ya mwaka 2014.
Vikundi vya kutetea haki za binaadamu vina shaka kuwa bi Haspel ameondoka nchini Thailand kwenda nchini Marekani kuendeleza mateso zaidi, lakini haijulikani ni jukumu gani alilitekeleza kiasi cha rekodi yake halisi kutambuliwa na CIA.

Hata hivyo inaarifiwa kuwa raisi Trump amesema Marekani itaendelea na mbinu hizo hizo za kumfunga mtuhumiwa wa ugaidi kitambaa usoni, akiwa amelala kwenye ubao na kutupwa kwa kasi kwenye kina cha maji huku mtu huyo akiwa ametanguliza kichwa .

No comments:

Post a Comment