Monday, May 7, 2018

MSIKITI WASHAMBULIWA WAKATI WA SWALA AFGHANISTAN


Maafisa kutoka Mashariki mwa Afghanistan wanaarifu kuwa watu kumi na nne wamekufa na wengine na kadhaa walijeruhiwa katika mlipuko kwenye msikiti katika jimbo la Khost.

Wamearifu kuwa mripuko huo ulitukia wakati watu walipokuwa wamejumuika kwa swala za adhuhuri.Mashuhuda wanaarifu kuwa msikiti huo ulikuwa ukitumika pia kama kituo cha usajili wa wapiga kura.

Kulikuwa na mashambulio kadhaa katika miji mingine tangu msimu wa usajili wa wapiga kura ulipoanza mwezi uliopita kwa uchaguzi wa bunge mwezi wa Oktoba mwaka huu, na mpaka sasa hakuna kundi lolote lenye msimamo mkali lililo jitokeza na kukiri kuhusika kwake.

Ingawa kundi la wanamgambo wenye msimamo mkali limetekeleza mashambulizi kama hayo hapo awali.Mnamo tarehe 22, mwezi wa nne , shambulio katika kituo cha kuandikishia wapiga kura katika mji mkuu Kabul liliua watu hamsini na saba.

Shambulio la mjini Kabul tayari kundi la wanamgambo wa dola ya kiislamu walikiri kuhusika nalo, ingawa mamlaka za Kabul zimetoa angalizo kwa watu kuwa wasijihusishae na uchaguzi ujao, ambao unaarifiwa kuwa ni mtihani muhimu wa uaminifu wa Rais Ashraf Ghani.Miongoni mwa waliojeruhiwa wanasadikiwa kuwa katika hali mbaya . Kumekuwa na matukio ya kushambulia vituo vya kupigia kura tangu msimu huo ulipoanza mwezi uliopita kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwezi wa October,kwa uchaguzi wa wabunge.

No comments:

Post a Comment