Monday, January 30, 2017

VIOLA DAVIS: Mwafrika wa kwanza kuwania tuzo 3 za Oscar

VIOLA Davis ndio Muigizaji wa kwanza mwanamke Mmarekani mwenye asili ya Afrika kupendekezwa kupokea Tuzo tatu za Oscar baada ya kupendekezwa katika kipengele cha Muigizaji Msaidizi Bora kutokana na umahiri wake wa kuigiza kwenye filamu “Fences.”
Sio mgeni katika kutengeneza historia, mwaka 2015 alikuwa ndio Mwanamke Mmarekani mwenye asili ya Afrika kushinda Tuzo ya Emmy katika kipengele cha Muigizaji Kiongozi kutokana na filamu ya drama “How to Get Away With Murder” akiigiza kama Annalise Keating. Viola alipendekezwa kwa mara ya kwanza kwenye tuzo za Oscar kutokana na filamu ya mwaka 2008 “Doubt” na alipendekezwa kwa mara ya pili kupokea tuzo hiyo mwaka 2012 baada ya kuigiza kama mfanyakazi wa ndani kwenye filamu “The Help.”
Muigizaji na mshindi huyo wa Tuzo Viola ameshajikusanyia tuzo kadhaa kwa sabbau ya filamu kama ‘Doubt’ na ‘The Help,’ pamoja na michezo ya filamu kama ‘King Hedley II’ na’Fences.’ Mwaka 2015, alikuwa ndio muigizaji wa kwanza Mmarekani mwenye asili ya Afrika kushinda Tuzo ya Emmy kipengele zha Muigaji Bora Kiongozi kutokana na Drama ‘How to Get Away With Murder.’ Mwanamama huyo alizaliwa South Carolina na kukulia Rhode Island, ambapo alianza kujifunza masuala ya uigizaji akiwa sekondari na kisha katika chuo cha Rhode Island.
Baada ya kuhudhuria Shule ya Sanaa ya Uigizaji ya Juilliard , Viola mara moja alianza kushiriki kuigiza michezo mwaka 1996. Alishinda Tuzo ya kwanza inayoitwa Tony mwaka 2001, na mwaka 2008 alipendeke zwa kwa ajili ya Tuzo ya Oscar kutokana na uigizaji wake kwenye filamu ya Doubt. Mwaka 2011, Viola alishiriki kwenye filamu ya drama inayoitwa The Help. Alishiriki pia kwenye filamu Ender’s Game (2013) na Get on Up (2014).
Viola alionekana tena mwaka 2014, ndani ya mfululizo wa filamu inayojulikana kama How to Get Away with Murder, na mwaka uliofuata alikuwa Mwanamke wa Kwanza Mmarekani mwenye asili ya Afrika Kushinda Tuzo ya Emmy. Muigizaji huyo alikulia eneo linalojulikana kama Rhode Island, alipenda filamu tangu akiwa mdogo. Baba yake alikuwa mtunza farasi. Mwanadada huyo alibaini ana kibaji cha kuigiza akiwa sekondari.Akiwa katika Chuo cha Rhode Island, Viola alitunukiwa Shahada katika masuala ya tamthilia mwaka 1988.
Kuanzia hapo aliendelea na masomo katika Shule ya Sanaa ya Uigizaji ya Juilliard mjini New York. Muda mfupi Viola alianza kujijen- gea jina mwenyewe ka- tika majumba na kumbi za maonesho na tamthi;ia mjini New York. Alianza kwa kuigiza katika tamthilia ya Seven Guitars mwaka 1996. Katika mchezo huo Viola anaigiza kama Vera mwanamke anarudiana na rafiki yake wa kiume aliyekuwa amekosana naye. Aliigiza tena mwaka 2001 katika Drama King Hedley II, ambayo umahiri wake wa kuigiza ulimuwezesha kushinda Tuzo ya Tony.
Katika skrini ndogo, Viola aliigiza kwenye tamthilia ‘City of Angeles’ , mwaka 2000. Pia ameshawahi kuwa muigizaji mualikwa kwenye tamthilia Law & Order. Mwaka 2008 viwango vya uigizaji vya Viola vilikuwa juu baada ya umahiri wake wa kuigiza ndani ya Doubt. Kwa mara nyingine alionesha uwezo wake na kuonesha anaweza kwenda sambamba na mastaa wakubwa Hollywood.
Katika filamu hiyo Viola anaigiza kama mama ambaye mtoto wake anaweza akawa amedhalilishwa kingono na Padre (nafasi iliyochezwa na Phillip Hoffman) katika shule ya Kanisa Katoliki aliyokuwa anasoma. Kutokana na kazi nzuri katika filamu hiyo, Viola apendekezwa kwenye Tuzo ya Academy kama muigizaji msaidizi bora. Mwaka 2011, Viola aliigiza sambamba na muigizaji Emma Stone, Octavia Spencer, Jessica Chastain na Bryce Howard katika filamu The Help filamu hiyo inahusu ubaguzi kati ya wake wa wazungu na wafanyakazi wa ndani Wamarekani wenye asili ya Afrika.
Katika filamu hiyo, Viola anaigiza kama Ailbileen, mfanyakazi wa ndani ambaye anahojiwa na mwandishi mzungu anayeitwa Skeeter aliyekuwa akiandika maisha ya wasichana wa kazi. “Wanawake katika hadithi hiyo ni kama mama na bibi yangu… wanawake waliozaliwa na kukuzwa Deep South, wakifanya kazi kwenye mashamba ya tumbaku na pamba, kutunza watoto wao na watoto wa wengine, kusafisha,’ anasema.
Akiwa Muigizaji Mmarekani mwenye asili ya Afrika, Viola aliendelea kutafuta nafati ya kuigiza zenye maana zaidi na huenda kuanzisha miradi yake binafsi. Mwaka jana alishiriki kwenye drama Suicide Squad na alitunukiwa Tuzo ya Golden Globe kwa uigizaji mahiri kwenye filamu Fences, sambamba na muigizaji Denzel Washington.
Baada kupata Tuzo ya Utendaji Bora katika nafasi ya Uigizaji Msaidizi , Viola aliitoa tuzo hiyo kwa baba yake kuonesha heshima ambaye muigizaji huyo alisema, “alizaliwa 1936, alitunza farasi na alikuwa na elimu ya darasa la tano…lakini ana hadithi na inastahili kusimulia.” Mwaka huu, Viola amependekezwa kwenye Tuzo za Oscar kutokana na filamu Fences. Viola anaishi mjini Los Angeles na mumewe Muigizaji Julius Tennon. Wanandoa hao pia mwaka 2011 wameasili binti anayeitwa Genesis.

No comments:

Post a Comment