Baada ya kuchelewa kambini kujiunga na kikosi cha timu ya taifa chini ya mika 20, Ngorongoro Heroes, Kocha wa kikosi hicho, Ammy Ninje amempata mbadala wa mlinda mlango Ramadhani Kabwili.
Ninje alimtema kwenye kikosi hicho mlinda mlango huyo kwa madai ya kuwa alichelewa kujiunga kambini na timu ili kujiandaa na mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON (U20) dhidi ya Mali.
Peter Mashauri kutoka JKU ya Zanzibar ndiye amechukua nafasi ya Kabwili ambaye alisafiri na kikosi cha Yanga kwa ajili kuelekea Algeria kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Ngorongoro Heroes watakuwa na kibarua Jumapili ya wiki hii, Mei 20 2018 kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam kwa ajili ya kufuzu kuelekea mashindano hayo ya AFCON kwa vijana.
Tayari Mashauri ameshajiunga na kikosi kambini ambapo sasa wanajifua kujiandaa kuwakabili Mali.

No comments:
Post a Comment