Saturday, April 28, 2018

YANGA YAWASILI JIJINI DAR

Kikosi cha Yanga kimewasili salama jijini Dar es Salaam kikitokea Morogoro kuweka kambi maalum kwa ajili ya Simba.

Yanga ilikuwa Morogoro kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya watani wao wa jadi, Simba, utakaopigwa kesho Jumapili katika Uwanja wa Taifa.

Yanga ina kibarua kigumu dhidi ya Simba ambao wamekuwa na kiwango kizuri msimu huu huku wakiwa kileleni kwenye msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 11.

Simba ipo kileleni ikiwa imejikusanyia alama 59 wakati Yanga ikiwa ina pointi 48 pekee huku ikiwa nyuma kwa michezo miwili.

No comments:

Post a Comment