Saturday, April 28, 2018

NGOMA NJE YA KIKOSI CHA YANGA

Taarifa zinaeleza kuwa Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Donald Ngoma, ameshindwa kujumuika na wachezaji wenzake kwenye kikosi kilichokuwa kimeweka kambi mjini Morogoro.

Mzimbambwe huyo hakuwepo kambini tangu kikosi hicho kiwasili mjini Morogoro mwanzoni mwa wiki na mpaka kinarudi jana Dar es Salaam hakuwepo.

Kukosekana kwa Ngoma kambini ni ishara tosha kuwa bado anasumbuliwa na majeraha hivyo ana asilimia kubwa ya kuukosa mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Uwanja wa Taifa.

Ngoma hajaonekana Uwanjani kwa muda mrefu kufuatia kuwa majeruhi ambaye amedumu nayo kwa takribani msimu mzima wa ligi.

Mara nyingi imekuwa ikiripotiwa kuwa ameshapona majeraha yake lakini mpaka leo hajaonekana dimbani kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment