Saturday, April 21, 2018

TSHISHIMBI KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA MBEYA CITY

Ikiwa imebakia siku moja timu ya Yanga kushuka katika dimba la Sokoine kuminyana na Mbeya City mchezo wa ligi Kuu, kiungo wao Papy Kabamba Tshishimbi hatoweza kushiriki mechi hiyo kwa sababu ya kupelekwa hospitali siku ya leo ili aweze kupatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyokuwa nayo.

Dkt. Bavu amebainisha hayo kupitia ukurasa maalum wa timu hiyo baada ya kurejea nchini wakiwa wanatokea Ethiopia katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

"Papy hatakuwa sehemu ya mchezo huo wa jumapili, aliumia Ethiopia, tukiwa kule tulimpatia matibabu ya awali, kesho atakuwa hospital kwa vipimo zaidi. Ibrahim Ajib atarejea kikosini kwa sababu amepona Maralia kuhusu Andrew Vicent hakuna shaka juu yake yuko vizuri anaweza kucheza ila itategema na waalimu kama wataona inafaa", amesema Dkt Bavu.

Kwa upande mwingine, Yanga imefuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufanikiwa kuitoa Welayta Dicha kwa ushindi wa jumla wa magoli 2-1.

No comments:

Post a Comment